GET /api/v0.1/hansard/entries/466772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 466772,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/466772/?format=api",
    "text_counter": 369,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Jambo la pili, katika Hoja kama hizi, ingekuwa muhimu kama Bunge lingehakikisha kwamba Miswada inanakiliwa wa Kiswahili ndiposa Wabunge waweze kuwazungumzia Wakenya kwa lugha ambayo sasa ni ya kitaifa. Fauka ya hayo, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu unahakikisha kwamba Wakenya wataweza kulipa kodi kwa njia sawia. Tunaona kwamba kutokana na vile vipengele vimependekezwa hapa, itakuwa ni rahisi kwa Serikali kupata ushuru kutokana na kampuni mbalimbali ambazo kwa muda zimekuwa zikikwepa kulipa ushuru na hususan kwamba wale ambao watakuwa wakikwepa kulipa kodi watakuwa wakichukuliwa hatua, hata kama wao ni meneja au wakurugenzi wa makampuni makubwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}