GET /api/v0.1/hansard/entries/466773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 466773,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/466773/?format=api",
"text_counter": 370,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Pia, kuna jambo ambalo linashangaza katika kipengele kimoja. Wakenya wana uzoefu wa kutafuta jinsi ya kujiimarisha kupitia mbinu kama vile Charity Sweepstake ama kubonyeza. Huu Mswada unasema kwamba ukibonyeza na ushinde, ni lazima ile kampuni ilipe kiasi fulani cha hizo pesa na pia wewe ambaye umeshinda, ulipe. Tunafaa kuwahurumia Wakenya kwa sababu wakilipa kodi kwa Serikali ilhali wenyewe pia wametumia hela kutafuta hiyo bahati na sibu, hili litakuwa ni jambo ambalo hawatalipendelea kwa kweli. Pia, huu Mswada unahakikisha kwamba ile Benki ya Afrika Mashariki imetiliwa maanani kama benki ya IMF na Benki Kuu ya Dunia. Hili ni jambo la kupigiwa upato kwa sababu litasaidia nchi husika ambazo ni wanachama kupata kuendesha miradi ambayo itaweza kuwasaidia wananchi wake. Ukiangalia zaidi pale, kipengele hiki kinaendelea kusema kwamba mali ya benki hii isiweze kutaifishwa kwa sababu, kwa ushawishi wa kisiasa, mambo kama haya yanaweza kutendeka."
}