GET /api/v0.1/hansard/entries/466774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 466774,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/466774/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashangaa kuona kwamba Mswada huu umependekeza kwamba asilimia 1.5 ya pesa ambazo Wakenya wanatuma kutoka nje ya nchi na mahali kwingi ambako wamekwenda kujitafutia riziki, zitozwe kodi. Pia, zile bidhaa za kinyumbani, kwa mfano, kama zimetolewa ngambo hususan na watu ambao wanarudi kutoka mataifa ya kigeni, zinafaa kutozwa kodi. Hili si jambo la kusifiwa. Wakenya wanatuma karibu Kshs1 billioni kila mwaka kuwasaidia wenzao ambao wamewawacha hapa wakienda kutafuta riziki kwingine na kutoza hizi pesa kodi kama vile ambavyo nimeelewa, basi ninafikiri hili si jambo ambalo litaweza kupigiwa upato. Pia, ile asilimia 10 ya kodi ambayo inatozwa katika mabenki, kuna kasheshe pale kwa sababu kuna fedha zingine ambazo pengine unawekeza tu katika akaunti, tofauti pengine unalipa kodi ya nyumba kila mwezi ama malipo kama hayo. Hili ni jambo ambalo sisi kama Bunge tunafaa kuangalia kwa kweli."
}