GET /api/v0.1/hansard/entries/466775/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 466775,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/466775/?format=api",
"text_counter": 372,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Ni jambo pia la kuimarisha moyo kuona kwamba hii sheria inasema kuwa kama mwaajiri anaweza kulipa bima kwa wafanyikazi wake, basi ataweza kupatiwa afueni kupitia mpango wa kodi. Hili ni jambo nzuri sana kwa sababu wafanyikazi wengi wamelemazwa katika shughuli za kikazi. Hilo jambo litahakikisha kwamba waajiri wengi wanatafuta bima kwa wale ambao wanawafanyia kazi. Huu Mswada pia unaweza kutusaidia sana kupunguza ugaidi kwa sababu unaharamisha zile mbinu ambazo zinaweza kutumiwa kutafuta hela za kufadhili shughuli za kigaidi. Pia, haitakuwa rahisi kwa watu kusafirisha fedha ambazo wamepata kutokana na biashara haramu. Kwa mfano, kuuza mihadarati. Hilo ni jambo ambalo limeangaziwa."
}