GET /api/v0.1/hansard/entries/467689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 467689,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467689/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika,kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao umejadiliwa na wenzangu. Bw. Naibu Spika, kwa miaka mingi au tangu tulipopata Uhuru, tuliona vile kiongozi wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya alivyotoa ahadi nyingi sana. Pia, kiongozi wa pili na watatu vile vile walipeana ahadi nyingi. Ahadi zenyewe zilikuwa kama kuambiwa kuwa kutakuwa na upanuzi wa barabara, kurekebishwa kwa reli, ujenzi wa shule na mengi ambayo hayajafanyika hadi wakati huu. Kadri tunavyoendelea, tunazidi kupata mambo yakusikitisha katika kaunti. Inadhihirika wazi upande wa akina mama. Watoto ambao wanazaliwa kabla ya muda unaofaa hawana nafasi ya kuishi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa kama incubators katika hosipitali zetu. Hii ni kwa sababu ya ukosefu wa pesa za kutosha katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, kuna hatari zingine ambazo kama hazitazingatiwa sawa sawa huenda zikazidi kuleta madhara kutokana na ukosefu wa pesa za kutosha katika kaunti. Tukiangalia jela zetu, utaona kwamba zina madeni makubwa ambayo mpaka wakati huu hayajalipwa. Wengi wa suppliers wa vyakula wamegoma kupeleka vyakula kwa sababu hawajalipwa. Nikizingatia Jela la Shimo la Tewa, kuna madeni ya ajabu na sasa suppliers wengi wamewacha kupeleka vyakula katika jela hiyo. Haya ni maswala ambayo yamechangia hata kuwa na ushoga katika seli. Inawabidi wafungwa walio na njaa kufanya visa viovu kwa sababu ya kutaka chakula kutoka kwa wenzao. Kwa hivyo, ukitaka nikupe chakula changu, lazima ufanye hivi ama vile. Haya yote yameletwa kwa sababu ya madeni na kutokuwa na vyakula katika jela zetu. Bw. Naibu Spika, tukiangalia congestion iliyoletwa na barabara huko kwetu Mombasa, haswa mahali kunakoitwa Kibarani – mahali ambapo kumetufanyia hata utalii wetu umezorota kabisa – mtalii atawasili nchini kupitia kiwanja cha ndege lakini hadi kufika hoteli, mahali ambapo panafaa kumchukua dakika 20 kutamchukua hata masaa manane. Yote haya yameletwa na barabara kutopanuliwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Laiti kungekuwa na fedha, upanuzi wa barabara ungekuwa umetekelezwa na barabara zetu Mombasa zingekuwa ziko sawasawa. Jambo hili linaleta hatari kiasi cha kwamba utakaa Kibarani kwa hata siku mbili na magari hayaendi, ilhali ukiyaangalia magari mengine, yamebeba vifaa vya hatari. Katika msongamano wa magari yale kuna watoto wa shule, abiria na watu wengine wengi. Hii ni hatari na yote haya yanaletwa na ukosefu wa fedha katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, wenzangu wametangulia kuongea kuhusu madeni. Mswada huu utakapopitishwa na pesa zitakapoingia katika kaunti, hofu yangu ni moja – madeni haya ambayo yanaongelewa mara kwa mara – yatalipwa na serikali za kaunti. Lakini lazima tujiulize kabla hatujayalipa, madeni haya yalikujaje? Je, madeni haya yaliwafaidi wananchi na kaunti? Je, tutayachukua madeni haya tukayalembezee Serikali kuu ama serikali za kaunti wakati yaliwafaidi watu wawili au watatu? Nikitoa mfano wa kwetu, Kaunti ya Mombasa, kabla ya kuingia katika Seneti, nilikuwa mwakilishi wa wadi katika"
}