GET /api/v0.1/hansard/entries/467693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467693,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467693/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nyingi, tumepata kuwa miradi ya jamii haifanywi. Kila tulipouliza, tuliambiwa kuwa manispaa iko na madeni. Na kila tulipofanya fujo tukitaka kujua madeni haya yameletwa na nini, tulikuwa tukiambiwa kuwa kati ya madeni hayo yalikuwa ya kulipa wafanya kazi mishahara. Leo, imeibuka ya kwamba wafanya kazi hawalipwi mishahara, miradi yetu ya jamii haifanywi na pesa zilitolewa na LATF pamoja na Serikali kuu. Je, pesa hizi zilipotelea wapi hapo katikati? Mswada huu utapita na nauunga mkono upite, kwa sababu utaenda kuokoa serikali zetu za kaunti. Lakini kitu ninachoomba ni kuwa madeni yatakayolipwa yawe ni madeni tunayojua yalifanya hiki ama kile. Lakini madeni ambayo hatutajua yalifanyiwa nini yafaa yalipwe na wale waliofaidika na madeni hayo. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono Mswada huu."
}