GET /api/v0.1/hansard/entries/467696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 467696,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467696/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nataka kuunga mkono Mswada huu wa ugawanyaji pesa. Kama tunavyoelewa, kulingana na kipengele cha 96 cha Katiba, sisi kama Seneti kazi yetu ni kulinda na kutetea rasilmali za zile kaunti tunazotoka. Ya pili ni kuhakikisha kwamba ugawanyaji wa pesa zitakazotoka katika Serikali kuu zimefika mashinani na zimefanya kazi inayohitajika kufanyika huko. Wakati ule Mswada wa pesa ulipokuja hapa, tuliona kwamba pesa zile zilikuwa hazitoshi, ndio sababu tukasema ziongezwe kutoka Ksh210 bilioni hadi Ksh258 bilioni. Lakini kwa ukosefu wa nidhamu ama kutozingatia masilahi ya serikali za kaunti, zile pesa zilipunguzwa ama zilibaki pale pale, Ksh210 bilioni. Hizi ni pesa kidogo sana zisizoweza kuleta maendeleo mashinani. Mimi natoka Kaunti ya Kilifi katika nchi yetu hii ya Kenya, na hivi karibuni, tulitangaza hizi kazi na tukasema zinahitaji wasomi. Tunaunga Mswada huu mkono kwa kuwa elimu itaweza kusambazwa vizuri ikiwa itawekwa chini ya mikono ya wale magavana walioko katika serikali za kaunti. Katika zile kazi zilizotangazwa, utaona ya kwamba mpaka ward administrator anatakikana awe ni mtu aliye na shahada ya chuo kikuu; dereva wa kupeleka gari anatakikana awe anajua mambo ya tarakilishi. Sisi tunauliza hivi; tangu lini dereva akajua mambo ya tarakilishi? Kazi ya dereva ni kupeleka gari, lakini hivi sasa tunaambiwa ya kwamba lazima kuwe na pre-qualifications zingine, kama awe na sijui ripoti ya Automobile Association (AA), awe na leseni ya class A, B,C,D na E; awe anajua mambo ya tarakilishi, na kadhalika. Hadi sasa, ni miaka zaidi ya hamsini tangu Uhuru upatikane; ugawanyaji wa pesa kutoka katika Serikali kuu umeweza kutunyima sisi, watu wa Pwani, nafasi ya kuwa na vyuo vikuu. Tunajua kuwa vyuo vikuu viko Nairobi na pande zingine za nchi, lakini haviko upande wa Pwani. Imewabidi watu waliokuwa na uwezo wa kusoma waje huku, pande za juu za Kenya na wengine watoke nje ya nchi ili kupata elimu ama kupata hizo shahada za vyuo vikuu. Lakini tukilinganishana hivi sasa, ikiwa hizo zitakuwa ndizo sifa zinazotakikana kwa muajiriwa, basi ni kumaanisha kwamba watu wengi wa Kilifi hawatapata kazi hizo kwa kuwa sio watu wote kutoka huko walio na shahada za vyuo vikuu. Bw. Naibu Spika, Mswada huu ni mzuri kwa sababu tumeona kwamba kunayo nia ya kuleta elimu karibu na wananchi wa huko mashinani. Hivi juzi tu, pia sisi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}