GET /api/v0.1/hansard/entries/467698/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467698,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467698/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tulibarikiwa kupata Chuo Kikuu cha Pwani kilichoko huko Kilifi, katika kaunti ninayowakilisha. Tumeanza, mwaka huu ama mwaka uliopita, kutarajia kwamba tutakuwa na wasomi wenye shahada za vyuo vikuu. Kwa hivyo, nasi pia tutakuwa na uwezo, iwapo kazi kama hizi zitatangazwa baada ya kama miaka miwili, mitatu ama mitano inayokuja; pia sisi tutakuwa tayari. Hata ukimwambia dereva awe na shahada ya chuo kikuu, hata sisi tutakuwa nazo. Bw. Naibu Spika, nikitoka upande wa elimu, nitaangazia suala la ardhi. Kama watu wa Pwani walipewa nafasi ya kumiliki ardhi zao kulingana na ugatuzi ama serikali za kaunti, ambazo tunajaribu kuzifanya zikithiri hivi sasa--- Tukiangalia Serikali ya kwanza tulipopata Uhuru mpaka sasa, ni miaka hamsini. Tumekuwa na Serikali ya Moi na ya Kibaki, lakini historia inatuambia ya kwamba watu wa Pwani waliokuwa wakiishi huko waliweza kukaa katika ardhi zao, lakini kuna mahali ambapo walikuwa hawaruhusiwi kukaa, na sisi tunaona kwamba hayo yalikuwa ni mambo ya kutugawanya. Tunaangalia habari ya zile maili kumi za upwao wa Pwani, ambazo hivi sasa, ikiwa hizi pesa zitaweza kutumika vizuri katika serikali za kaunti; na ikiwa hizi pesa zitaweza kusaidia kulingana na mipangilio iliyoko katika serikali za kaunti, basi wale watu wanaoishi katika sehemu zile waweze kutengewa pesa na kupewa hati za kumiliki ardhi. Hali kadhalika, pesa hizi zitatumika kuhakikisha kuwa yale mashamba yaliyokuwa yamesemekana yapo katika ule mshipi wa Pwani wa maili kumi, ambapo watu wengine wanaishi mpaka hivi sasa, hizo pia zisiwe jukumu la Serikali kuu. Tunajua kuwa maraisi wote watatu waliotangulia walipewa uwezo wa kutoa mashamba kama hayo yaliyoko katika ufuo wa Pwani. Wagiriama na watu wote kutoka sehemu zote za Pwani wanaishi huko na hawana ruhusa ya kumiliki hiyo ardhi iliyo huko ufuoni wa Pwani. Mtu anakuja na barua na kusema “hapa ni kwangu; tokeni nimepewa ardhi hii.” Tunauliza hivi; kwani hiyo ilikuwa ni ardhi ya watu wa Pwani ama ilikuwa ni ardhi ya mtu mmoja binafsi kuweza kutoa kama zawadi? Hilo ni kosa lililofanyika na ni lazima kosa hilo lirekebishwe. Tunashukuru ya kwamba sasa, katika Katiba, tuko na"
}