GET /api/v0.1/hansard/entries/467700/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467700,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467700/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na tunatarajia wataangazia dhuluma hii iliyofanyiwa watu wa Pwani ili kutakapokuwa na ugavi wa mashamba kama hayo, wale watu waliokuwa wakiishi huko wapewe ardhi hizo kulingana na hizi sheria za serikali za kaunti. La mwisho ninalotaka kugusia pia, Bw. Naibu Spika, ni kusema kwamba watu wa Pwani pia wapewe nafasi katika nyadhifa mbali mbali za Serikali kuu. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba hivi leo, ni watu wachache kutoka Pwani ambao wamepewa nyadhifa za juu katika Serikali kuu. Ni kama watu wa Pwani hawako tena; ama vile watu kule nyumbani wanavyosema, kuwa kila sisi tukijaribu kuwaambia kuwa Pwani ni Kenya, wao wanasema Pwani si Kenya; na hii ni sababu ya dhuluma kama hizi!"
}