GET /api/v0.1/hansard/entries/467706/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467706,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467706/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, nataka kuunga mkono na kusema kwamba Mswada huu ni mzuri na utaweza kuleta maendeleo, hasa tukihakikisha kwamba wale magavana ambao wako katika utawala wa serikali za kaunti wasitusiwe. Tumeona hivi majuzi kwamba wanaitwa sijui “maraisi.” Ukiitwa “his Excellency,” wewe sio raisi; unaitwa “ his Excellency the Governor ;” haukuitwa “ his Excellency the President .” Lakini tukiangalia watu wengine – kwa sababu wanajaribu kuharibu majina ya hawa watu walio pale – wanaanza kutumia lugha isiyofaa. Mimi nasema ya kwamba magavana wetu wanafanya kazi nzuri, na kulingana na utawala wao mpaka sasa, naona ya kwamba wanafanya vizuri. Kwa hivyo, wapewe nafasi wafanye kazi zao lakini si matusi. Naomba kuunga mkono Mswada huu."
}