GET /api/v0.1/hansard/entries/467707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467707,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467707/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, asante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu wa Ugavi wa Fedha kwa Kaunti. Ninasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu ni wa maana sana kwa wananchi wote. Mimi sina shida na ugavi lakini matumizi yake yananitia wasiwasi. Hapa tunawakilisha kaunti mbalimbali hapa nchini. Kwa hivyo, tunajua shida zinazowakabili watu wetu. Kwa mfano, kaunti nyingi zina barabara mbaya, ukosefu wa zahanati na hospitali, upungufu au ukosefu wa maji safi na kadhalika. Akina mama hutembea masafa marefu wakitafuta maji safi ya kunywa. Hospitali ziko mbali sana. Kwa hivyo, ninapozungumza nitaegemea sana upande wa matumizi ya pesa ambazo zitapewa kaunti mbalimbali hapa nchini. Ni jukumu letu kama viongozi kujihusisha katika matumizi ya pesa hizi. Inafaa tuelimishe wananchi ili pesa hizi zitakapofika kule mashinani zitumiwe kwa njia iliyo bora zaidi. Ninapozungumza hapa watu wetu wana shida nyingi. Kuna wale ambao walitimuliwa kutoka msitu na kwa sasa wanaishi kando ya barabara. Hema walizopewa miaka sita iliyopita zimeraruka. Wanaishi katika mazingira duni; wakati wa masika wananyeshewa. Watoto wao wanashikwa na magonjwa kwa sababu ya baridi kali kwa maana hawana nyumba. Watoto hawana chakula cha kutosha. Watu hawa kwa sasa wanaishi katika hali ya umaskini mwingi. Kwa hivyo, shida yangu si kiasi cha pesa ambacho kitapewa kaunti, lakini jinsi pesa hizo zitakavyotumika. Ninaomba pesa hizi zitumike kwa njia nzuri. Ni mapenzi yangu kuona kuwa viongozi wote katika kaunti wamejihusisha na kuhakikisha pesa hizi zinatumika kwa maendeleo. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}