GET /api/v0.1/hansard/entries/467789/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467789,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467789/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Watu hawafahamu mambo ya ufugaji kwa sababu ya magonjwa yanayowakumba wanyama. Magonjwa haya yamewafanya watu wetu wasiwe na mifugo kama vile watu wa Kaunti ya Samburu na kwingineko. Sisi sote hapa mtakubaliana nami kwamba hakuna chakula kinachofurahisha Wakenya kuliko nyama. Nadhani wengi wetu saa za mchana walikula vipande vya nyama. Hata tukitoka hapa kwenda katika nyumba zetu, pia tutakula nyama. Hii ni Hoja ambayo kila mmoja ataifurahia na sote tunafaa kuiunga mkono. Tupende tusipende, katika harusi ama matanga, tunachinja ng’ombe au mbuzi. Tunafaa kujiuliza wanyama hawa hufugwa wapi na ni vipi tutaendeleza ufugaji huu ili tule nyama nzuri kila siku? Ningependa kusisitiza kama ndugu yangu Sen. (Dr.) Khalwale alivyosema tuwe na vyuo vya utafiti ili tuboreshe nyama, ngozi na mifupa ya mifugo yetu. Bidhaa hizi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}