GET /api/v0.1/hansard/entries/467793/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 467793,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/467793/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "lakini sisi tunawaita wafugaji wa kurandaranda. Kama tunavyoimba katika wimbo wa Taifa, tuungane mikono, pamoja kazini, ningependa kusema tuungane mikono katika kaunti zetu. Ningependa kutoa changamoto kwa sehemu zingine ambazo zina ardhi zenye rutuba. Ikiwa tutazingatia kuwa ndugu zetu Wasamburu ni wafugaji lakini hawana malisho, tunafaa kuchukua jukumu la kuwasaidia kupanda ama kukuza kilimo ambacho kitawasaidia wanyama wale. Nafikiri huenda kikawasaidia pakubwa wafugaji wa kuhamahama kuweza kutulia mahali pamoja na kulisha wanyama wao. Wakati wanyama wale watakaposhiba nina hakika kuwa hata visa vya wizi wa mifugo vitapungua. Hii ni kwa sababu wizi wa mifugo unaletwa na watu wa kupenda kufuga na hawana mifugo ya kutosha. Kutokuwa na mifugo wa kutosha ni kwa sababu hawana chakula cha kuwalisha. Kwa hivyo, wanyama hawazaani inavyotakikana. Hii huleta hamu ya kuiba. Hii ndio maana kila wakati tunasikia kuwa Wasamburu wameuwana kwa sababu ya mifugo. Nafikiri wanahitaji kusaidiwa katika ukuzaji wa chakula na pia mifugo wale washibe na wazaane. Bw. Naibu Spika, nafikiri pia kuwa swala hili linatakikana kutiliwa maanani kwa sababu ukosefu wa chakula na wizi wa mifugo ndio umechangia Tana Delta kuwa na mauaji. Kila mmoja anataka shamba yenye rutuba na maji. Hilo swala limewafanya watu wa jamii za Orma na Pokomo kuuana. Bw. Naibu Spika, kule kwetu Pwani tuna minazi mingi sana, lakini ukitembea kwa maduka makubwa utapata coconut milk kutoka Thailand. Serikali kupitia kwa Wizara ya Kilimo inafaa kuzingatia ukuzaji wa mnazi na kuwahamasisha Wapwani na inafaa kuwaonyesha faida ya mnazi. Mnazi unatoa makuti ya kujengea paa na mafuta inayosaidia kutengeneza sabuni. Vile vile unatumika kutengenezea virembesho kama vile vipuli na shanga. Pia unatengeneza kileo ambacho kinatupa usingizi mzuri usiku na doormats. Leo hii tungekuwa na duka kama Nakumatt ama Uchumi ambalo linauza bidhaa mbalimbali za mnazi pekee yake, wapwani leo tungekuwa wapi? Serikali ingepiga marufuku kuletwa kwa nyama za mikebe kutoka nchi za nje na kuwahamasisha wafugaji kuhifadhi nyama kwenye mikebe, zingetusaidia wakati wa njaa. Lakini kazi yetu ni kuimarisha biashara ya nchi za nje kwa kuleta nyama za mikebe ambazo zimekaa kwa miaka mingi. Tunajiletea maradhi makusudi ilhali tunaweza kutengeneza hiyo nyama hapa. Bw. Naibu Spika, ningependekeza pia kuwa barabara katika sehemu ambazo wafugaji wanaishi zitiliwe maanani. Hii itahakikisha usafiri salama wa mifugo hao. Hata hivyo, sisitizi kuwe na barabara hizi kwa sababu nataka nyama wasafirishwe, bali ningependa vichinjio vitiliwe maanani. Hii ni kwa sababu pia wanyama wakisafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, wanadhoofika njiani na nyama yao huwa haina ladha. Sio kama mnyama aliechinjiwa kule malishoni. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa kutilia maanani hivi vichinjio ili tutakapokuwa katika makao yetu ya sterehe, tunapokula nyama ya kuchoma na kuiteremsha na bia moja ama mbili, hiyo nyama iwe ni tamu. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii kwa sababu mimi ni mlaji mkubwa sana wa nyama."
}