GET /api/v0.1/hansard/entries/468387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 468387,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/468387/?format=api",
    "text_counter": 246,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gertrude",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante Sana, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Ninaifurahia Hoja hii sana. Hata hivyo, mchango wangu utakuwa ni mfupi sana kuhusiana na Pwani ninakotoka. Swala la kilimo ni nyeti sana katika Mkoa wa Pwani. Jambo hili limekuwa likihuzunisha na kukera watu wetu kwa miaka mingi. Ardhi ya Pwani ina rutuba nyingi sana. Kuna watu wanaoamini kuwa Wapwani ni wavivu na si wakulima. Ningependa kusema kwamba wapwani ni wakulima hodari sana. Lakini shida yetu ni kuwa ardhi kubwa yetu imemilikiwa na absentee landlords . Jambo hili limefanya sisi kutotilia maanani shughuli za kilimo kwa sababu hatuna mashamba. Ningependa Serikali yetu ihakikishe kuwa mashamba haya yamepewa Wapwani. Serikali inaweza kuwapa mbegu na vifaa vingi vya kilimo ili watu wetu waweze kulima. Pwani inaweza kukuza chakula kingi ambacho kitawasaidia watu wa sehemu zingine nchini. Bw. Naibu Spika, kuna kilimo cha njaa marufuku. Hiki ni kilimo ambapo akina mama wanakuza chakula katika magunia. Wanajazaa magunia mchanga na kupanda mimea kama vile sukumawiki, mboga na kadhalika. Hii ni njia mojawapo ya kusaidia kupigana na njaa katika nchi hii. Ukulima huu unawezakupewa kipao mbele na akina mama wakuze chakula kingi nje ya nyumba zao. Ningependa kuwahamasisha akina mama wa Tononoka kukuza chakula kwa njia hii. Kupitia katika kikao hiki cha Seneti, ningependa kusisitiza kwamba Pwani kuna ardhi yenye rutuba. Shida yetu kubwa ni kwamba Serikali imetunyima mashamba ya kulima. Wakati wa maonyesho ya kilimo ya Mombasa, Serikali hujishughulisha sana na kuwaonyesha watu wa Pwani, hasa Mkomani, kupanda sukumawiki juu ya mawe. Mkomani ni mahali ambapo kuna mawe matupu lakini utapata ule ndio wakati Wizara ya Kilimo itazingatia Pwani ikionyesha watu jinsi ya kupanda cabbage na sukumawiki juu ya mawe. Jambo hili linanikera sana kwa sababu wao huja tu wakati wa maonyesho. Wakati mwingine wako wapi? Hauwezi kuwaona mashambani wakiwaonyesha watau wa Pwani mbinu mbalimbali za kilimo. Hii ni kwa sababu Serikali haitilii maanani ukulima katika nchi hii. Nashangaa kwa nini sehemu zingine ukulima unatiliwa maanani sana kuliko Pwani. Ni lazima ukulima katika Pwani uzingatiwe kikamilifu. Nimesema hapo juu kuwa ardhi yetu ni yenye rutuba. Lakini ardhi kubwa ya Wapwani inamilikiwa na"
}