GET /api/v0.1/hansard/entries/469805/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 469805,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/469805/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ili kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza, ningependa kuiunga mkono. Bw. Naibu Spika, Hoja hii ni nzuri kwa sababu imekuja wakati unaofaa. Huu ni wakati wa kuthibiti kaunti zetu. Wakati kama huu kuna haja ya kuboresha mambo ya kielimu katika kaunti zetu. Ikiwa ni hivyo, kile tunataka sisi ni tuwe watu wa kwanza kufaidika na mbinu za kuweza kuleta vyuo vikuu karibu na watu ili iwe ni rahisi kwa watoto kuweza kusomea katika vyuo vikuu. Tunataka kuwapa nafasi wale walioko katika shule za upili kuiga mfano wa wale ambao watakuwa wakisoma katika vyuo vikuu hivyo ili kuweza kufanya bidii na kuwa na tamaa ya kujiunga na vyuo vikuu kule mashinani. Jambo hili litasaidia katika kuimarisha uchumi wa sehemu ambazo vyuo vikuu vitakuwa. Yule atakayekuwa na mbuzi wake ataweza kuuza, mwenye mboga zake ataweza kuuza kwa sababu kutakuwa na wanafunzi na wahadhiri wengi ambao watakuza uchumi wa sehemu hiyo. Bw. Naibu Spika, kama vile wengi walivyosema, si makosa ya watu wa sehemu fulani kwamba sehemu yao imebaki nyuma kimaendeleo. Ni vizuri tujifahamishe na historia ya nchi hii. Kutoka wakati wa ukoloni, kulikuwa na mipango, ikianzia na ya reli iliyowekwa kuanzia Mombasa hadi Kisumu na Laikipia, sehemu ambao Wazungu walikua wakikaa. Kwa hivyo, ilivutia wafanyakazi wengi, hasa kutoka mikoa ya Magharibi na Nyanza, ambao walikua wakifanya kaza aidha kama wapagazi ama kwa Wazungu. Kwa hivyo, kulikuwa na nafasi ya watu kuweza kusoma wakati huo. Lakini sisi watu wa Kaskazini Mashariki, hasa ile sehemu iliyojulikana kama “ NorthernFrontier District ” (NFD) – ambayo ilijumlisha sehemu za Lodwar, Samburu, Isiolo, Garissa, Wajir, Mandera, Moyale na Marsabit – ilibaki nyuma kimaendeleo. Shule ya kwanza iliyoanzishwa na Serikali ya ukoloni ilianzishwa 1948 kule Isiolo. Baada ya hio, ikahama ikaenda Garissa katika mwaka wa 1949 na mwisho ikapelekwa Wajir. Na watoto hawa katika hizi wilaya zote, walikua wakienda Wajir kupata masomo ya shule ya upili. Sehemu zingine za nchi, wamishenari ndio walianzisha elimu – hata si Serikali ya Ukoloni. Wale ambao walikua katika dini ya Ukristo walikuwa na nafasi nzuri ya kuweza kusoma katika shule hizo. Isitoshe, Bw. Naibu Spika, hii Sessional Paper No.10 ilitengezwa na afisa wa upangaji wakati Waziri wa Mipango alikuwa Tom Mboya. Tom Mboya alitoka wapi? Yeye alitoka Mkoa wa Nyanza. Yeye alipanga kuwa nyanda za juu za Kenya ndio zitafanyiwa maendeleo zaidi kuliko zile sehemu ambazo zilisemekana sio productive kwa Kizungu; yaani hazizalishi kitu chochote ambacho kinaweza kusaidia uchumi wa nchi hii. Isitoshe, tuchukue kalamu na karatasi tuangalie Wizara ya Elimu ilikua inaongozwa na nani. Seneti hii inatakikana iwaunganishe Wakenya wote kutoka sehemu zote za nchi. Na kama kuna shida, tuizungumzie pahali ilipo bila ya sisi kuzungumza juu ya sehemu fulani ambayo inalenga kabila fulani. Hiyo haitakua vizuri kwa sisi. Ni lazima tuwe na mfano mzuri kwa wananchi wote wa Kenya. Sisi tunataka kuwaunganisha Wakenya wote ila si kuwatenga wengine kama mjadala huu unavyowalenga watu kutoka Mlima Kenya na kwingineko. Mimi sitoki Mlima Kenya, lakini ukweli lazima usemwe; watu wa sehemu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}