GET /api/v0.1/hansard/entries/470006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 470006,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470006/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa familia ya marehemu kutoka kwa familia yangu na watu wote wa Pwani, hasa wazee wa Kaya. Ningependa kutoa sababu ambazo zinasababisha watu kufa. Napenda sote hapa tujue kwamba sote tu maiti watarajiwa na kifo hakikosi sababu. Hii ndiyo sababu Malaika watatu walitumwa kuja duniani na mission. Walitembea na kwenda mpaka ilipofika saa kumi na mbili jioni ikaingia giza na hawakuwa wamefika mahali walituma na Mungu. Walifika mahali palipokuwa na nyumba ya nyanya na babu na wakatarajia kukaribishwa lakini wakakataliwa. Waliendelea na safari yao katika nyumba nyingine kuomba mahali pa kulala lakini wakakataliwa. Mwisho, walifika mahali ambapo kulikuwa na vilema wawili. Waliwanyenyekea ili wawape mahali pa kulala lakini wakakataa. Walifika mahali pa tajiri; mwenye mali, magari na kila kitu na wakamwomba awape mahali pa kulala hata kama ni kwa basement ya kuweka gari lake lakini wakakataliwa. Lakini askari alimbembeleza yule tajiri ili awaache walale hata kama ni kwenye basement chini na mwisho tajiri akakubali. Wale malaika watatu walilala pale walikuwa in the form of wanadamu. Usiku, wale malaika wawili wadogo walimwona yule malaika mkubwa akichimba mahali. Alipomaliza, walimwona akichoka akiziba. Asubuhi, malaika wakamwuliza, ulikuwa ukifanya nini? Yule malaika aliwaambia, nilikuwa nikimtengenezea huyu tajiri mahali. Nitawaelezea sababu yake. Walitoka na kuendelea na safari yao kuelekea kule Mungu alipokuwa amewatuma. Walienda na ilipofika saa kumi na mbili ikielekea saa moja, kulikuwa na baridi na mvua ilikuwa imeanza kunyesha, wakafika kwa masikini wengine na wakaomba mahali wakaribishwa walale. Walikaribishwa na masikini akawaambia; ingieni kwangu. Nina kitanda kimoja. We will share . Sisi tutalala chini, ninyi laleni kwenye kitanda kwa sababu ninyi ni wageni na mmetoka mbali. Walipewa chakula wakala halafu wakalala. Lakini asubuhi, malaika Yule mdogo alipoamka na kuchungulia nje, alipata mtu na mkewe walikuwa wamekaa nje wakilia. Aliwakaribia na kuwauliza, kwa nini mnalia? Walisema, sisi, katika maisha yetu tumekuwa na ng’ombe mmoja tu na ndio tulikuwa tukimtegemea kwa sababu ya maziwa ili tuuze maziwa na watoto wetu wasome na ndio kila kitu kwetu. Leo, ng’ombe wetu amekufa. Yule malaika ndogo alikasirika sana. Aliingia ndani na kumshika malaika mkubwa na kumwuliza ni kwa nini alimwacha yule ng’ombe afe ilhali ana mamlaka ya kusimamisha kufo. Yule malaika mkubwa alitoka na kwenda kwenye yule ng’ombe. Aliwaangalia na kuwaambia malaika wenzake; yule ng’ombe amekufa lakini ilikuwa ni bwana ya mama huyu ambaye alikuwa afe. Lakini, mimi nime plead na Mungu na kumwambia afadhali umchukue ng’ombe. Angalia tumeenda kwa tajiri na akatunyima mahali pa kulala lakini masikini ametukubalia. Aliwageukia wale malaika wadogo na kuwaambia; kila kifo huwa na sababu. Nyote mlio hapa ni maiti watarajiwa na kila mtu atakuwa na sababu ya kufa. Tutatafuta kila sababu ambazo zimemchukua marehemu lakini nataka kuwaambia kuwa kila kifo kina sababu. Malaika mdogo alimwambia malaika yule mkubwa, tulipokuwa kwa tajiri, ulikaa usiku mzima ukimzibia mahali palipokuwa pamebomoka na akamwambia hakuwa akiziba. Kuanzia ile siku, pale mahali nilipoziba ilikuwa mahali alikuwa akiweka utajiri wake. Ni dhahiri kuwa hata pesa zake haweki katika benki, anaweka katika shimo lile. Nililiziba na kunzia ile siku, yeye ni masikini. Aliziba mali yake yote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}