GET /api/v0.1/hansard/entries/470360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 470360,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470360/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "The Senator for Machakos County",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": " Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii niliopata ili niweze kuchangia kuhusu Hotuba ya Rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya. Bw. Spika, nimemsikiliza kwa makini sana Kiongozi wa Wengi katika Bunge letu la Seneti. Ni haki yake kusifu na kuchangia yaliosemwa huko, lakini kuna kiini cha kuangalia ikiwa yaliosemwa ni ya haki na yanaweza kutumizwa au ni kurudia maneno yalioyosemwa katika taifa letu miaka 50 iliyopita. Bw. Spika, mhe. Rais alipokuwa akiwaniani kuwa Rais wa tatu wa taifa hili mwaka wa 2002, niliandamana naye kwa ndege kwenda kufanya kampeni za urais. Tulipaa juu ya Mto Athi, na tukiwa juu aliniuliza: Je, unafikiri kutatua tatizo la maji katika taifa letu na hasa sehemu za Ukambani na kuelekea Pwani ni nini? Nilimjibu kwamba kiini cha kutatua matatizo hayo ni kulinda Mto Athi na Mto Tana kwa sababu maji yanayopita pale kati ya miaka 50, tukikumbuka kwamba blueprint ya kwanza ambayo ilitoka na ilikuwa ya Rais wa kwanza ilikuwa ikisema kwamba mwaka wa 2000 kila nyumba itakuwa na maji ya mfereji katika taifa letu. Baada ya hayo, nilishangaa sana wakati Rais wa nne alipozungumza kutatua tatizo la maji na hakusema kwamba atafanya juhudi kuona kwamba maji yanayopita Mto Athi na Mto Tana hadi Mombasa hayatafungiwa yote, lakini yatapunguzwa kiasi na kutumiwa katika sehemu hizo. Alirudia maneno ya Rais wa kwanza, Rais wa pili na Rais wa tatu kwamba yuko tayari kutatua tatizo la maji, lakini bila kuonyesha vile atakavyolitatua tatizo hilo. Bw. Spika, ni kweli na ni dhahiri kwamba Rais alihutubia Taifa na kusema kwamba mitambo ya tarakilishi (laptops) itapewa watoto wa miaka saba. Ilikuwa ni kicheko, sarakasi na kasheshe ya maneno tu. Mheshimiwa Spika, nilifika kwako The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}