GET /api/v0.1/hansard/entries/470362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 470362,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470362/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nikitafutia mrengo wa CORD kura na ninachoweza kufanya kwa sasa ni kuomba Mungu tu, ili watoto wa sehemu ambayo unatoka wewe na sehemu ambayo ninatoka kama watapata laptops hizo, Mungu awajalie. Kwa sababu hakuna jambo ambalo ni la aibu kuamua kwamba, baba yangu, mama yangu nami mwenyewe hatujaendesha gari au baiskeli halafu unatuambia kwamba utatupatia barua tuende DT Dobie tuchukue gari la aina ya Mercedes Benz tuende nayo nyumbani. Utakuwa unatuchekelea tu. Kwa hivyo, pesa zinazotengwa kwa ajili ya kununua tarakilishi kwa watoto, kama tuongee ukweli, hiyo itakuwa kama kashfa ya Anglo Leasing nyingine. Mtu ambaye anataka kuuza mitambo yake na inapitishwa hapa na mheshimiwa spika, ninakuambia tarakilishi ambazo zitanunuliwa hazitakuwa na thamani. Huo utakuwa ukurasa wake. Maisha yake yamepita na haifai hata kutumika katika kueleza barabara ambayo itakayokanyagwa na watu. Bwana Spika, katika Hotuba yake, Rais alisema kwamba---"
}