GET /api/v0.1/hansard/entries/470369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 470369,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470369/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "The Senator for Machakos County",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": " Bw. Spika, Rais wa nne wa Kenya katika kampeni zake alisema kwamba laptops hizo zitafika baada ya siku 100 kutoka siku atakapoapishwa. Taarifa yake na mazungumzo yake hapa inasema laptops hizo zitaingia katika mwezi wa Januari. Huu ni ushauri ambao unaona kwamba Wakenya hawajui hesabu. Ningetaka kumwambia kwamba tangu aapishwe, mwezi wa nne, mpaka Januari mwaka ujao, itakuwa zaidi ya siku mia mbili. Hii ni kusema kwamba siku 100 zitakuwa zimepita. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa yeye ni kiongozi ambaye ameteuliwa na wananchi wa Kenya na ametoa ahadi zake. Mimi sikuchaguliwa na watu wa Machakos County ili nije hapa kusikiza maneno na kuwapelekea. Hivi sasa, tunataka uwezo wa kufanya na kuona kwamba mambo yanafanyika. Kiongozi wa Wengi katika Seneti amezungumzia kuhusu uchaguzi ambao ulikuwa wa maana na ulifaa sana. Alizungumza na kusema kwamba upanuzi wa Serikali ya Muungano iliyopita ulitokana na tamaa na watu kutaka kushirikishwa katika Serikali. Ni dhahiri kwamba muungano wa Serikali iliyopita ulitokana na ulanguzi wa kura na kura kufanyiwa ukarabati. Kama kura zingewekwa sawa sawa, hakungekuwa na muungano wa Serikali iliyokuwa awali. Mheshimiwa Raila Odinga angekuwa rais wa nchi hii na hakungekuwa na Serikali ya muungano. Muungano ulitokana na wale waliokarabati kura. Tunajua Serikali iliyoko sasa iliingia kimungu mungu kwa sababu tulishuhudia na kuona kwamba wale ambao walikuwa na akili na uwezo walikuwa na waakilishi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}