GET /api/v0.1/hansard/entries/470387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 470387,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470387/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbuvi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 80,
"legal_name": "Gideon Mbuvi",
"slug": "gideon-mbuvi"
},
"content": "Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. Je, Seneta Muthama yuko sawa vile anavyoendelea kupotosha Bunge hili kwa kusema kwamba Serikali iliyopita imepuuza eneo la Ukambani bali yeye mwenyewe alikuwa Kinara katika Serikali iliyopita? Makamu wa Rais, katika miaka mitano ya Serikali iliyopita alitoka sehemu ya Ukambani. Kuna viongozi wapya kutoka sehemu ya Ukambani ambao wamechaguliwa ambao watatatua shida hiyo. Mimi natoka Ukambani. Kangundo kuna stima na barabara sawa. Kwa hivyo, tusifanye unafiki. Rais Uhuru hajamaliza miaka miwili katika Serikali. Kwa hivyo, hatufai kumsulubisha Rais Uhuru kwa makosa yaliyofanywa na rais wengine. Kila Wizara ilikuwa na bajeti yake. Wizara ya Barabara ilikuwa na bajeti yake."
}