GET /api/v0.1/hansard/entries/470784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 470784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470784/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Nakushukuru sana, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. (Dkt.) Khalwale. Naamini kwamba madhumuni na makusudi ya Hoja hii ni kuweka adabu, heshima na vile vile kulinda mali ya umma. Bw. Spika wa Muda, sisi wanasiasa katika taifa letu tumeshuhudia mambo ambayo yanaudhi sana; mojawapo ni kwamba vyama vimetengezwa kama kampuni za kibiashara. Vyama hivi vinatengezwa kulingana na ukabila. Nataka nikuhakikishie kwamba yale makabila madogo madogo katika nchi yetu hayana vyama kwa sababu viongozi katika makabila haya, wakijipima wanaona kwamba hata wakiunda vyama, hawawezi kufika mahali. Jambo la kuudhi katika taifa letu ni kwamba vyama hivi vyote vimetoka katika yale makabila makubwa. Ukienda sehemu za Ukambani, Ukikuyuni ama hata zile sehemu za Wakalenjini, hapo ndipo utapata vyama vitano, kumi, ishirini na zaidi. Wananchi wamenyanyaswa na kugawanywa na hivi vyama. Ni kwa sababu gani wagawanywe? Hii ni kwa sababu madhumuni ya kwanza kabisa ya vyama hivi ni kuuza vyeti vya kuwania viti wakati wa uchaguzi na kufanya biashara. Jambo la pili, Bw. Spika wa Muda, ni kwamba uchaguzi ukiisha, kuna pesa ambazo zinatolewa na Serikali kwa vyama hivi na kila chama kitakwenda kudai kigawiwe pesa hizo. Kwa hivyo, tusipochunga, nikisikiza vile ndugu yangu, Sen. Murkomen, alikuwa akiongea, sio chama hiki au kile. Hatuko hapa kuangalia ni chama gani ambacho kina watu wengi, na ni chama gani ambacho kina maadili ya kuwafaidi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}