GET /api/v0.1/hansard/entries/470786/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 470786,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470786/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Wakenya. Lakini tunatakiwa kujiuliza; je, tutaweza kufanya nini ili vyama vilivyo katika taifa letu viunganishe Wakenya pamoja? Bw. Spika wa Muda, wewe ukiwa katika kaunti yako ya Migori, unajua kwamba unaongea sawasawa na Sen. Muthama akiwa katika Kaunti ya Machakos; na unaongea na Sen. Omar akiwa katika Kaunti ya Mombasa kwa sababu tumeungana kama Wakenya katika chama kimoja. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, ninayokusudia kusema ni kwamba naunga mkono mjadala huu, lakini namtaka Sen. (Dkt.) Khalwale ajue kwamba tutapendekeza mabadiliko Fulani wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Seneti katika vipengele fulani. Kwa sababu gani? Ikiwa chama kitakuwa kinapokea pesa kwa sababu ya kuwa na Mbunge mmoja, Seneta mmoja ama mwakilishi wa wanawake mmoja, hesabu hiyo itakuwa ngumu. Tutakuwa tunatengeneza na kueneza vieneza na vyama vya kuwagawanya Wakenya. Tunataka kuenda sambamba na mapenzi ya Wakenya. Ni lazima sasa tufanye kazi bila kuangalia kabila zetu na pia bila kuangalia mtu anatoka wapi na chama chake kinaelekea wapi. Tunafaa kufanya kazi ambayo itawaleta Wakenya pamoja. Kwa hivyo, kaunti zetu zote 47 zinafaa kuungana. Nakubaliana na mapendekezo kwamba kura za Rais zinafaa kuondolewa katika mbinu ya kugawa pesa za kisiasa katika taifa letu. Chama cha URP, kwa mfano, kiko katika mrengo mmoja na TNA. Chama cha URP hakikumweka Rais mamlakani. Kura ambazo wangeweka katika sanduku ya Urais ziliwekwa katika debe ya TNA. Kwa hivyo, kama kura hizo zitahesabiwa kupitia kwa Rais ambaye alichaguliwa na TNA na chama cha URP kiwe nje, hakutakuwa na usawa. Nakubaliana na hayo. Kura za Urais zinafaa kutoka kwa makadirio ya watu ambao walipiga kura na kufikiria vile pesa zitakavyogawanywa. Tukiwa na chama ambacho kina Wabunge 60 kutoka sehemu ya kati, pia, hakifai kupewa hela. Chama ambacho kinawakilishwa katika kaunti 47 za taifa la Kenya kimewaleta wawaakilishi katika Seneti na pia katika Bunge la Kitaifa, kinafaa kupewa pesa. Chama ambacho kimewaleta Wabunge fulani kutoka Meru peke yake hakifai kupewa pesa. Chama ambacho kina Wabunge kutoka Ukambani peke yake kinapewa pesa za nini? Tunataka kupanua nchi ili tuwe na usawa. Watu wengine wako katika vyama ambayo havijasajiliwa. Watu hao wanafaa kuungana na Wakenya wengine katika vyama ambavyo vitapewa pesa. Leo, nimeona watu ambao wako katika vyama ambavyo havijasajiliwa wakisema wanataka kujiunga na CORD ili wapate pesa. Wametupa ahadi kwamba baada ya kupewa pesa, wataungana nasi kupiga kura. Hiyo ni njia ya kuwagawanya Wakenya. Mimi nazingatia umoja wa Wakenya. Mkamba akiunda chamba chake, nitasema hicho ni chama cha kuigawa nchi. Ikiwa Wamaasai wataunda chama chao, tutasema wanagawa nchi. Tunafaa kujua kwamba chama ambacho kinajulikana na ambacho kina Wabunge wawili, basi hakiendi mahali popote. Ndugu zangu Sen. Sang na Sen. Murkomen hukaa na kuzungumza katika lugha yao nikiwa nimekaa karibu nao karibu kwa masaa mawili. Wao huzungumza katika lugha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}