GET /api/v0.1/hansard/entries/470788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 470788,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/470788/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "yao hata kama mimi sielewe kitu. Hawana aibu. Mimi nikikaa na Sen. Mutula Kilonzo Jnr., pia tunazungumza hivyo hivyo. Sen. Orengo akiwa na Sen. Kajwang pia wanaongea vivyo hivyo. Sisi hatujakomaa katika mambo ya lugha ambayo itatulete pamoja. Bado tuko katika misingi ya ukabila. Sen. Omar Hassan kutoka pwani ametoka jamii ya Wabajuni. Jamii hiyo haijulikani. Mtu kama huyu ataunda chama lini ambacho kinaweza kumfanya ajulikane kabisa katika taifa hili? Akitoka nje, watu watasema chama chake kina mtu mmoja na vyama vya Wakikuyu ndivyo vina watu wengi. Bw. Spika, wewe huwezi kuwa hata na ndoto ya kuitawala taifa letu kwa sababu hauna jamii kubwa. Ukizungumza katika mkutano kwamba unataka uongozi wa nchi hii, utaulizwa maswali mawili. Kwanza, utaulizwa watu wako ni wangapi? Pili, hata ukitaka uongozi wa chama, swali la kwanza ni una watu wangapi? Baada ya swali hilo, pia utaulizwa una watu wangapi? Kenya imepiga hatua katika mambo ya ukabila. Mambo haya yanaanzia hapa. Tulipokuwa na uchaguzi mkuu, chama cha UDF – Sen. Khalwale atanisamehe – kiliundwa ili kura kutoka sehemu za Western zisiende kwa chama kingine. Hata kama ungejipamba vipi na kujaribu kujiunga na chama cha watu wa Western, ili uwanie kiti cha Rais, haungeweza. Hata kama kungekuwa na nini, haungepewa kura hizo. Pesa zitapelekwa katika vyama vya jamii kubwa na hapo ndipo wizi wa pesa za umma utakuwepo. Chama kikiundwa, kitapewa pesa. Atakayekuwa akitoa pesa hizo, atakuwa amezitoa wapi? Hii ni mali ya umma ambayo imeibiwa."
}