GET /api/v0.1/hansard/entries/472405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 472405,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/472405/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanaoathirika zaidi ni akina mama ambao wanawapoteza watoto wao. Watoto pia wanawapoteza baba zao ambao wanawapa riziki za kila siku. Bw. Spika, hatuwezi kuendelea hivi. Kama vile nilisema hapo awali katika Seneti hii, hata wanyama katika nchi hii hawako salama tena. Najua kwamba mambo ya kujiuzulu sio desturi yetu kama Wakenya, lakini kila siku watu wanakufa. Tumemsikia hata Waziri ambaye amepewa jukumu la usalama akisema kwamba uvamizi haukutekelezwa na kikundi cha Al Shabaab bali ni wanasiasa. Kisha akasema tena kuwa sio wanasiasa waliohusika bali ni mauaji ya kawaida. Tumechoka na mambo haya. Nasikitika kwamba hata Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika Seneti amesema kwamba amefika mwisho. Ameomba watu wamjibu lakini hapati majibu hayo. Tunajua kwamba amefanya kazi katika Wizara ya Usalama kama Waziri. Sijui akina mama ambao wako kule Turkana, Lamu na kwingine watafanya nini. Bw. Spika, sisi kama Seneti ni lazima tufuate zile kanuni ambazo zilikuwa zimependekezwa na Waziri wa Usalama za kuhusisha Magavana katika maswala ya usalama. Ni lazima tujue jambo hili limefika wapi. Kama Seneti, tunafaa kujua kwamba tunahitaji kushirikiana katika---"
}