GET /api/v0.1/hansard/entries/473660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 473660,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/473660/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Pia, Mswada huu unazungumzia ushirikiano baina ya vitengo vya Serikali vinavyoangalia mambo ya waathiriwa kutokana na majanga ya uhalifu. Kwa mfano, kuna kitengo cha polisi na kitengo cha mahakama. Mara nyingi watoto wetu ambao wameathiriwa kwa sababu ya kubakwa ama kwa kufanyiwa mambo machafu na mabaya kama vile ya ngono huwa wanakosa kupata haki kwasababu vitengo hivi havina ushirikiano dhabiti. Unapata polisi katika uchunguzi wao na ushahidi unakuwa na utata na mahakama inapata ripoti ambayo haitaweza kumsaidia mtoto yule. Lakini wakati vitengo hivi vitakuwa na ushirikiano dhabiti basi mtoto huyu atapata haki yake na anapopata haki, basi hata sisi Wakenya tunatoa shukrani sana."
}