GET /api/v0.1/hansard/entries/473664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 473664,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/473664/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ninaunga mkono na ninatoa kongole sana kwa mhe. Millie linahusu kuweka mtoto katika hali ya usalama wakati ameathirika. Tumeona mifano katika nchi yetu. Unapata baba wa kambo anambaka mtoto wa mkewe. Wakati anatenda kitendo hiki, anaenda mahakamani, anapewa bond na anatoka nje. Akiwa nje na akina mama ni sisi, wengine tunawapenda waume wetu, unaona kwamba huwezi kuwa kando na mme wako. Unaendelea kuishi na mme wako na mtoto huyu anapolegeshwa katika familia kuishi na mama na baba wakambo aliyembaka, hawezi kupata haki. Huyo mtoto ataendelea kuathiriwa zaidi na mambo mengine. Basi ikiwa tutawapeleka katika taasisi za usalama ambapo watawekwa sawa, wapate chakula, makao na matibabu, basi watoto hao watajua haki zao zitapatikana katika njia ambayo inahitajika."
}