GET /api/v0.1/hansard/entries/473669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 473669,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/473669/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Jambo la mwisho ambalo ninatoa kongole kwasababu limenifurahisha sana katika Mswada huu ni lile la kuzungumza katika lugha ambayo utaielewa ama lugha ambayo umeichagua. Tunafahamu kwamba lugha za taifa ni mbili, nazo ni lugha ya Kiingereza na lugha ya Kiswahili lakini unapata watoto na akina mama wengi katika mashinani wanapenda kuzungumza katika lugha yao. Hii pengine ni lugha yake ya Kikuyu, Kidigo au Kiluhya ili aweze kuzungumzia yale mambo ambayo yamemvika yeye kama Mkenya. Hivyo basi kukiwa na mkalimani, tunaweza kusikia yaliyojili katika mikasa kama hiyo."
}