GET /api/v0.1/hansard/entries/473674/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 473674,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/473674/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, Waheshimiwa ambao wako nyuma yangu wana mkutano mwingine. Ninakuomba uwakanye. Bi. Naibu Spika wa Muda, kuna watu tunaowawakilisha ambao wanateseka. Shida iliyoko ni kwamba hawana nafasi ya kujitetea; hawajui pa kuelekea ili kupata usaidizi. Ningependa kusema hivi: Ikiwa wewe ama mimi tutanajisiwa hakuna mtu atajua katika nchi nzima kwa sababu sisi ni wabunge. Kuna wengi ambao wamepata shida lakini wamenyamaza kwa sababu hawajui wataambia nani. Kuna visa vingi vya mama na watoto wake wasichana kunajisiwa na kuporwa mali. Hawa ni watu hawana watu wa kuwafariji na kwa hivyo wanasumbuka. Tunashukuru sana kwa ajili ya huu Mswada kwa sababu hii sheria itawasaidia watu kama hawa. Wapo wale wanaosumbuliwa na wenye pesa. Mtu akipigwa ama auliwe na mwenye pesa humu nchini huwa ni shida kubwa kwa sababu mnyonge hana lake. Kutokana na huu Mswada, tutaweza kuwakumbuka wanyonge na kuwasaidia. Pakitokea maafa kama yale yanayojulikana kama “ bomb blast ” na mengineyo sharti tukumbuke kwamba kuna Wakenya wasio na sauti. Itakuwa ni furaha yetu sisi sote ikiwa sauti zao zitasikika kwa sababu ya huu Mswada. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}