GET /api/v0.1/hansard/entries/474849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 474849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/474849/?format=api",
    "text_counter": 66,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Nikimaliza, iwapo polisi wanasema wanataka kufanya uchunguzi wa kiafya kwanza, ama kutumia mbio kama mbinu inayoonyesha ni kurutu gani bora, katika Bura, daktari ni mmoja, na ndiye anakagua makurutu 100. Je tutazuiaje ufisadi? Nikimaliza, Bw. Kavuludi alisema yeyote mwenye malalamishi ampelekee lakini karani akasema kwamba mwenyekiti hachukui malalamishi yoyote. Tunataka mbinu badala ya kupeleka malalamishi kwa sababu kuna mchezo wa paka na panya. Inafaa kuwe na tume huru ambayo itachunguza jambo hili. Wale wanaoajiri ni tume ya Kavuludi. Itajichunguza vipi? Afadhali malalamishi yaende kwa Kamati ya Bunge maanake walipokuwa wakiajiri, walisema hawataki maoni ya wanasiasa. Kwa vile ufisadi umedhihirika, wacha wanasiasa wauchunguze."
}