GET /api/v0.1/hansard/entries/475357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 475357,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475357/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "lake. Yeye alitukumbusha mambo machache hapa na pale hasa kulingana na mawazo yake mwenyewe, ambayo anayaona kule kwao Rwanda. Alitukumbusha shida walizokuwa nazo mwaka 1994 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda. Wakati huu, karibu Watutsi milioni moja waliuawa kwa sababu ya uzembe wa ukabila. Hii ni hali ambayo haiwezi kuruhusiwa au kukubalika kuingia katika taifa letu. Tunajua kwamba huko Rwanda, makabila haya mawili yanaongea lugha moja. Sisi hapa tuko makabila 42 ukiongeza mengine machache; labda, tuko 45 kwa sababu Wahindi ni kabila, tunaongea lugha tofauti. Tuna sera na mawazo tofauti. Kwa hivyo, tuna shida zaidi kuliko zile zilizokuwepo kule Rwanda, na ni lazima tutahadhari kabla ya hatari. Lakini hata hivyo, jukumu la mambo hayo siyo kwa mwananchi peke yake lakini hasa kwa viongozi. Inafaa viongozi wa Taifa hili la Kenya wawe na mawazo mazuri yaliyokomaa na ya uongozi halafu wasiwe na siasa kali. Viongozi wetu wamejificha ndani ya vyama vyao vya kisiasa na hawataki kuelekezwa. Wamekuwa kama popo ambaye hupenda kupumzika akiwa ameelekeza kichwa chini. Na labda kwa sababu ni kipofu, popo anafikiria kwamba kila mnyama analala hivyo. Ukijaribu kumkumbusha popo aruke kidogo ili alale vizuri, ndio ataruka na labda atakutupia kinyeshi, lakini atarudi na alale vile ulivyompata. Hivyo ndivyo walivyo viongozi wetu na mawazo yao. Bi. Spika wa Muda, juzi kulikuwa na mambo ya uwiano; kuongea tu juu ya mawazo tofauti. Viongozoi wa Taifa waketi chini na kuongea mambo kuhusu nchi yao. Huyu akikubali, mwingine anakataa, huyu akigeuza mawazo na kukubali, yule mwingine anakataa. Wamekuwa kama popo. Lakini wale wanaojeruhiwa ni wananchi. Wao wamepata vinono na wanakula. Hawafikirii hali ya raia wa kawaida. Wamekuwa kama kuku na mwewe kwa sababu dua la kuku halimdhuru mwewe. Wakati mwingine, kuku atalia kwamba vifaranga wake wameliwa, lakini wakati huo mwewe naye anamshukuru Mungu kwa kupata kitoweo. Mungu ataamua nini kwani huyu anashukuru na huyu mwingine analia? Kila mtu anafikiri ni haki yake. Hivyo ndivyo tulivyo hivi sasa. Wale walioko kwenye utawala wanaona ni vyema wafanye hivyo ilhali wale wa upinzani wanalia. Haya ni mambo ambayo ni lazima tutafakari tukiwa wananchi na viongozi hasa, nchini na kufikiria kwamba, je kesho lawama itakuwa upande gani? Wakati wa kuunda hii Katiba mpya ambayo tunaifurahia, mimi nilipinga na nikasema kwamba tuirekebishe kwanza ndipo tuipitishe. Wengine wakasema kwamba tuipitishe na tuirekebishe baadaye. Baada ya kuirekebisha na kupata unono na uhondo ndani ya Katiba, wamesahau kwamba kuna mambo yalioyohitajika kurekebishwa kwa sababu wana mamlaka; wana vinono, wananyonya na wamesahau. Inafaa wote tuitikie mwito tulioambiwa na watu wakati ule wa kuongea mambo ya ratiba ya Katiba. Wote tulikubaliana kwamba kuna mambo mabaya ndani ya Katiba. Ni njia ya kuirekebisha tu ndio tuliotofautiana; tuipitishe turekebishe baadaye, turekebishe sasa ndipo tuipitishe. Wakati huu, ni lazima wote tukubaliane kwa dhati kwamba kuna dosari ndani ya Katiba ambayo huenda ikafanya uongozi wa Taifa la Kenya kuwa mgumu. Inafaa wote kukubali kwamba ni sasa. Kama kuna jambo linafaa turekebishe sasa, tusingoje kesho, kwa sababu majuto ni mjukuu. Lakini iwapo kwamba tumesahau kwa haraka, basi kuna shida. Tunapigwa kulia na kushoto na kule Mombasa hamna biashara. Ndio kuna ukabila, lakini The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}