GET /api/v0.1/hansard/entries/475359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 475359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475359/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ni kwa sababu ya kutosikiza mawazo ya wengine. Tuna shida hiyo kwa sababu tumejitumbikiza kwa shida za taifa la Somalia, tukawa wakombozi halafu tumekatalia huko. Hivyo basi, wanalipisha kisasi. Sisi tutavumilia tu kwa sababu kila wakati tumekuwa wavumilivu. Bi Spika wa Muda, ni nini hasa chanzo cha matukio haya? Juzi tulidokezewa kwamba siyo al Shabaab bali ni viongozi wasiotosheka ambao wanafanya maafa na kuonekana kwamba ni al Shabaab . Kama ni hivyo, inafaa wapelekwe gerezani. Makachero wako wapi watuambie ni akina nani wanaofanya mambo hayo? Vifo vya wananchi visiwe tu ni stakabadhi za kusema kwamba kumi wamekufa leo, ishirini wamekufa kesho, elfu moja kesho kutwa na hakuna lolote linalofanywa. Wakenya wanamwaga damu na viongozi wanacheka tu. Wanaitumia kama jambo la siasa. Taifa la Rwanda ni kielelezo cha kuonyesha ni wapi madhara kama haya yanaweza kufika. Wao wamejipiga mioyo konde, kutafakari, kuongea wenyewe kwa wenyewe na kuona ni wapi walikosea. Hivi sasa wanajenga taifa la kujivunia na sisi sasa tunaanza kujifunza kutoka kwao. Taifa la Rwanda linaanza kutufundisha mpaka hata vitu vidogo kama usafi. Tunaenda Rwanda kuona vile mji mkuu wao unawekwa safi. Hii ni aibu kubwa. Wakenya wemejaa kule Rwanda. Wao ndio viongozi wakuu wa biashara na Serikali, walioajiriwa kwa mikataba. Sera hizo zote ni fikira za Wakenya, lakini huku nyumbani ni kama seremala anayeunda kiti kizuri lakini kwake hana kiti. Mwingine akikalia kiti alichokiunda vizuri--- Mkurugenzi Mkuu wa Kilimo kule Botswana alikuwa ni Mkenya. Aliimarisha kilimo mpaka wakaanza mifugo na kuwa taifa kuu la ulimwengu ambalo linauza mifugo kwa faida kuu. Lakini huku nyumbani kilimo cha mifugo kinakufa, mpaka hata kiwanda cha Athi River kimefungwa. Hii ni aibu. Je, uzalendo uko wapi? Ni jukumu la kila Mkenya, mdogo kwa mkubwa, kuwa na fikira ya uzalendo. Sikubaliani na mawazo ya Mzee G.G. Kariuki. Hatufai kusahau kwamba kuna wale wanyonge ndani ya taifa la Kenya. Kuna jamii ndogo ndogo ambazo zimefinywa. Isije ikawa ni hadithi ya mwewe na kuku. Mali inapogawanywa wanyonge wanawachwa. Kuna Mkuria mmoja tu aliyewahi kuwa Waziri kwa miezi kadhaa na ni mimi. Kuna Mkuria mmoja tu aliyewahi kuwa Balozi. Hatujawahi kuwa na Officer CommandingPolice Division (OCPD) wala Provincial Commissioner wakati ule. Ukiangalia Kenya nzima wale walio wachache ndio wameathirika ndani ya Serikali. Je, hatufai kulia? Tutalia na kusema: “Wakubwa, mnapokula hata makombo tuachie kwa sababu sisi pia ni wananchi wa Kenya. Barabara zinapojengwa, tunafaa kukumbukwa pia, kwa sababu sisi pia ni wananchi wa Kenya na tunalipa kodi licha ya unyonge wetu.” Kwa hivyo ni kweli kuwa kuna wale ambao wamefinywa. Ni lazima wale walio wengi wafikirie wale wanyonge, kwa sababu hawana kura za kutosha kuwa na Rais kutoka kwao. Hata nafasi za Mawaziri zikigawanywa hawawezi kupewa kwa sababu ni wachache. Tusije tukasahau kwamba ni jukumu letu sisi tukiwa viongozi kujua kwamba wanyonge na masikini wapo nchini. Lakini pia sisi tukiwa viongozi tusikarisike tukikumbushwa. Nakumbuka wakati mwingine nilianza kusoma na kutafsiri Katiba. Nilipomaliza kutafsiri na kusema mawazo yangu, nilitupwa korokoroni kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}