GET /api/v0.1/hansard/entries/475361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 475361,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475361/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "nimesema mambo mabovu. Wakati ule nilikuwa nasema mambo ya National Land Commission (NLC), nikitafsiri kitabu cha Serikali. Naomba hotuba yangu itangazwe kwa wananchi ili waone kama kweli mawazo yangu yalikuwa mapotovu na hate speech . Niliyoyasema yanatokea sasa hivi. Lakini kwa sababu nilikuwa mnyonge nilitupwa. Kwa sababu nilikuwa Serikalini wakati ule na nikasema “No” wakati Serikali ilikuwa unasema “Yes”, ilibidi nitupwe ndani ili niwe kielelezo cha kuwafinya wengine wasije wakathubutu kufanya hivyo. Mawazo ya Mkenya wakati wowote yanafaa kusikilizwa yawe madogo au makubwa, kwa sababu funzo hilo laweza kuwa ndilo lenya manufaa zaidi Kenya nzima. Labda baadaye mkifiria kuhusu jambo hilo kwa undani, mtagundua kwamba lingeokoa au kuongoza nchi na kuifanya kuwa na fanaka, bahati nzuri na mavuno mema. Kwa hivyo tunapoongea kuhusu Hotuba hii, tukumbuke Afrika ya Mashariki. Ni lazima tuwe wa kwanza kukubali na kutekeleza kipengele cha tano cha mkataba unaongoza Afrika Mashariki. Tulikuwa na Tanzania, Uganda na Kenya, kisha tukaungana na Rwanda na Burundi. Nakumbuka mambo haya yakitekelezwa nikiwa Waziri wa mambo Afrika Mashariki."
}