GET /api/v0.1/hansard/entries/475380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 475380,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475380/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda. Nashukuru kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia Hoja ya Hotuba iliyotolewa na Rais wa Seneti ya Rwanda katika Bunge hili la Seneti ya Kenya, Mheshimiwa aliyekuwa hapa. Jina lake ni nzito sana. Ninajaribu kulitamka lakini nashindwa. Nilikosa kuhudhuria kikao cha Seneti jana lakini leo, nitasema machache kuhusu yale ambayo alisema. Niliipokea Taarifa yenyewe na pia nilielewa ujumbe ambao alitoa. Nchi ya Kenya iko mbele kwa maendeleo katika eneo letu la hapa Afrika Mashariki. Taifa la Kenya linaheshimika kwa sababu ya tabia ya Wakenya; ujuzi wao na vile walivyo wakakamavu kwa sababu wao hufanya mambo yao kama Wakenya. Msimamo wetu na ujasiri wa Wakenya unatambuliwa. Ukienda Uingereza, Ujerumani na Amerika, utawapata Wakenya ambao wanafanya kazi huko. Wakenya hawa wana heshima sana. Taifa la Rwanda, lilipojikomboa baada ya kukumbwa na vita vya wao kwa wao na kumwaga damu na ukabila, lilitegemea taifa letu la Kenya sana. Lugha yao ya kitaifa wakati huo ilikuwa Kifaransa. Lakini sasa, lugha inayozungumzwa sana ni Kiingereza. Ni Wakenya ambao walichangia kukuza Kiingereza katika nchi ya Rwanda. Pia, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}