GET /api/v0.1/hansard/entries/475382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 475382,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475382/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "madaktari Wakenya na wahudumu wengine wa ofisi ambao walikuwa na ujuzi tofauti walipata kazi za juu huko. Spika wa Seneti ya Rwanda aliyezungumza hapa hakutaka kutufurahisha kwa mambo ambayo sio halisi. Ukweli wa mambo ni kwamba kama angetaja mengi kuhusu Kenya, angesema kama sio Kenya, ingekuwa vigumu kwa Rwanda kujimudu na kuwa mahali ilipo sasa. Ikiwa Wakenya hao wanaheshimika hivyo, swali ni kwa nini Wakenya wakiwa hapa kwao hawaheshimiwi? Wakenya ambao wamefanya kazi katika mataifa ya nje hawajapelekwa kortini kwa mashataka ya kujaribu kuiba ama kupokea rushwa. Tukiwa nje, hiyo ndio tabia yetu lakini tukirudi nyumbani, tunakuwa kama tumeoza. Waswahili husema, mcheza ngoma kwao hutuzwa, Ni kitu gani kinachotukera tukiwa hapa? Na ndugu yangu Sen. (Prof.) Kindiki yuko hapa. Ni mmoja wa wale ambao walichukuliwa kwa heshima kubwa katika hiyo korti. Hakuna pahali Mkenya alisimama na kukashifiwa kwa kutojua sheria. Hadi leo, wale Wakenya walioko katika hiyo korti wanaheshimika sana. Hata sisi tunaona kwamba matamshi ambayo yanapewa kipaumbele ni yale ambayo yanaheshimika. Lakini swali ni: Ni kichaa gani au kasheshe gani inawapata Wakenya wakiwa hapa nyumbani kwao? Wakenya ambao wanafanya kazi katika Wizara ya Fedha kule Rwanda wanahakikisha kwamba pesa za Serikali ya Rwanda zinatumika vizuri kuambatana na kazi zilizotengewa. Hapa kwetu mwaka wa matumizi ya pesa za Serikali unakwisha bila sisi kutumia zaidi ya Kshs387 bilioni. Hii ni aibu kubwa. Kwa hivyo, ikiwa hao wenzetu ndio wanapanga vile pesa za nchi nyingine zitatumika, basi kwa nini mwaka nenda, mwaka rudi, pesa za nchi ya Kenya hazionekani ni kazi gani zimefanya? Ni nini kinachowakera Wakenya? Wananchi wa Rwanda wanafanya kazi tofauti na sisi na kuhakikisha pesa zao zinatumika vilivyo. Wakati umefika kwa sisi Wakenya kuamua barabara tutakayoifuata ili tuwe na maendeleo katika nchi hii. Bi. Spika wa Muda, mataifa yanaotuzunguka yanataka kuiga mfano wetu. Sisi tuko mbele sana kwa mambo mengi, hasa siasa. Tunaweza hata kutangaza siku ya Saba Saba ambayo inawafanya watu wengine kukosa usingizi. Sisi tunawatia mori sasa Watanzania. Siku hizi wanaweza kusimama na kuzungumza kama sisi. Kwa sababu kabla vyama vingi vya kisiasa kukubalika hapa nchini, Kenya tulifanya kazi ngumu sana. Hata Sen. Mugo alifanya kazi kubwa sana kwa sababu alikuwa mmoja kati ya wale waliokuwa mstari wa mbele ili kuona ya kwamba nchi hii ina vyama vingi. Nchi kama Tanzania ilikuwa na chama kimoja tu. Waliweza kubanduka na kupiga hatua mbele baada ya kuona kwamba Kenya imepata mrengo wa vyama vingi vya kisiasa. Hii ni kuonyesha kwamba sisi ni kama taarifa ya kusomwa na mataifa yanayotuzunguka. Ili tufaulu na tusiwe baba ambaye analisha watoto wa nje, lakini kwake nyumbani watoto wanalala njaa, ni lazima tutimize matakwa yetu kwanza. Bi. Spika wa Muda, ikiwa magazeti zetu ndizo zinazosomwa sehemu ya Afrika Mashariki, na inaonyesha kwamba wakati wa matumizi ya pesa za Serikali unaisha bila sisi kutumia pesa zilizotengewa miradi fulani hapa nchini, sisi tutakuwa kweli mfano mzuri wa kuigwa na mataifa mengine. Mimi nitajichukia sana ikiwa tutaanza kuiga mambo ya maendeleo kutoka kwa wananchi wa Rwanda ambao tumeliwafundisha mambo mengi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}