GET /api/v0.1/hansard/entries/475384/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 475384,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475384/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ni juzi tu Taifa la Rwanda linaanza kuimarika. Lakini ukitembelea nchi zingine, unaambiwa kwamba inafaa Kenya ijimudu kwa shughuli zake ili ikae kama Rwanda. Leo inasemekana kwamba Rwanda ndio nchi safi kabisa katika eneo hili letu. Swali ni: Je, ikiwa watu walipigana kuuana na kuchinjana, waliwezaje kusafisha miji yao na ikawa na heshima kutuliko, ilhali sisi ambao tulikuwa mstari wa mbele na hatujakuwa na matatizo kama hayo? Nchi ya Rwanda inatoshana na Kaunti ya Machakos. Hii ni aibu kuba sana. Uongozi wa Taifa hili ni lazima ukome kuwatetea watu wafisadi kutoka makabila yao. Ni lazima hatua kali ichukuliwe dhidi ya watu hao ili nchi yetu tuheshimiwe na mataifa mengine. Ni lazima ukweli usemwe. Ni lazima Wakenya wote wapewe nafasi za kazi kama Wakenya. Hatutaki kuona kabila moja likipendelewa na kupewa nyadhifa kubwa Serikalini. Bi. Spika wa Muda, nchi ya Rwanda imeweza kufaulu kwa sababu Rais Kagame ni mjasiri wa kuamua mambo bila mapendeleo ya kikabila. Yale makabila yaliokuwa yakipigana hayapigani tena baada ya Rais Kagame kuchukua hatamu za uongozi. Lakini angelikuwa ni mtu anayeogopa na kuzingatia mambo yasiyo ya ukweli, Rwanda haingekuwa vile ilivyo hivi sasa. Kwa hivyo, ni aibu kubwa sana kwa Wakenya kuambiwa wafanye mambo yao vile wananchi wa Rwanda wanavyofanya kwa sababu wanazidi kutushinda kimaendeleo. Hapa nchini Kenya tunataka kuona usawa katika Serikali yetu kulingana na Katiba yetu. Lakini vile mambo yalivyo hivi sasa, utumishi wa umma katika taifa letu umepewa kabila moja. Kuna kabila nyingine inayofuatia kwa karibu kwa kunusanusa ilhali Kenya ni nchi ya watu 40 milioni. Wakati Rais wa zamani wa Rwanda alifanya kazi kwa misingi ya kikabila, watu waliuana na kuchinjana kama kuku. Lakini baada ya kuzingatia heshima na ujasiri wa maamuzi, Rwanda imekuwa nchi moja. Tunataka kuona usawa katika Serikali. Hatutaki kuona kama, kwa mfano, Kamati ya Ulinzi wa Kitaifa ikifanya mkutano, unahesabu watu tisa kutoka kabila moja katika wanakamati 11. Watu wawili pekee yao ndio hawaelewi ni jambo gani linaloendelea katika mikutano yao. Sisi tukitarajia kwamba askari wetu wataleta ulinzi katika Taifa letu. Watawezaje kuleta ulinzi katika nchi yetu ikiwa wakiamka asubuhi kwenda kazini wanakashifiwa kwamba wanafanyia kazi kundi fulani la watu hapa nchini. Kwa hivyo, sisi tunaongea maneno ambayo yataleta upendo nchini Kenya na uhusiano wa Wakenya. Ikiwa tutaungana na Wakenya wengine walioko mataifa mengine na kuwahusisha katika utumishi wa umma katika taifa letu, tutaweza kuleta amani nchini Kenya. Kuna swali moja ambalo ninajiuliza: Inakuwaje askari wetu wananyang’anywa bunduki na wakora? Ikiwa askari wetu ndio wanaouwao, ilhali wao ndio wanaofaa kutulinda, ni nani aliye na usalama hapa nchini?"
}