GET /api/v0.1/hansard/entries/475392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 475392,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/475392/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, hakuna kitu kama hicho. Kama anataka nihesabu ninaweza kufanya hivyo. Je, Mkuu wa Majeshi ni nani? Je, Mkuu wa Idara ya upelelezi ni nani? Je, Mkuu wa National Intelligence Service (NIS) ni nani? Tunaweza kuwahesabu. Mimi sitaki aibu hapa. Mhe. Seneta anafaa kuelewa kwamba mambo ninayoongea ni ya Kenya. Mimi nilikaa na Sen. Beth Mugo na kukubaliana kwamba ni lazima tumsaidia Rais Mwai Kibaki alete usawa katika taifa letu. Kwa hivyo, siipotoshi Seneti hii hata kidogo hapa. Sisemi mambo ya uongo. Bi. Spika wa Muda, ikiwa kuongea kuhusu mambo haya ndio kuleta ukabila, basi ni nani atakayesimama na kukataa ukabila?"
}