GET /api/v0.1/hansard/entries/476236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 476236,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/476236/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nasimama kumpongeza Rais wa Seneti ya Rwanda, Dr. Jean Damascene Ntawukuliryayo kwa Hotuba yake jana ambayo haikuwa mrefu lakini ilikuwa ya maarifa. Siku chache zilizopita, tarehe 3-07-2014, nilikuwa na bahati kuwa Rwanda walipokuwa wakisherehekea maadhimisho ya ukombozi wao ambao wanaita Kwivohora kwa Kinyarwanda na nikaweza kushirikiana na Wanyarwanda. Hata mhe. Rais wa nchi hii ambaye ni Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliweza kuhudhuria sherehe hizo. Bw. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba kuna mambo mengi ambayo tunaweza kujifunza kutoka nchi ya Rwanda. Pia kuna mambo mengine ambayo hatufai kuyaiga kutoka nchi ya Rwanda. Niliweza kuhudhuria makumbusho ya mauaji ya halaiki ya watu yaliyotokea miaka 20 iliyopita. Nchi ya Rwanda wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo kama nchi ingawa ni wachanga kidemokrasia. Katika Hotuba yake Rais huyo alisisitiza uongozi wa akina mama. Kwangu, hilo ni jambo la muhimu kwa sababu nchi ya Rwanda ina ongoza ulimwenguni kwa kuwa na wanawake wengi sana katika Bunge lao. Hiyo ni asili mia 64 ambayo haijawahi kuonekana nchi nyingine za dunia. Tulikuwa kule na akina mama tukihudhuria mkutano ambao ulikuwa umewaleta pamoja wanawake Wabunge kutoka nchi zaidi ya 70. Bw. Spika wa Muda, napenda sana kusoma lugha za kitamaduni za Kiafrika na za hapa nchini. Wasomali wako na msemo mmoja kuwa ukidungwa mishale miwili, mmoja kwa jicho na mwingine kwa tako, jambo la busara la kufanya ni kutoa ule ambao uko kwa tako ndio uweze kuketi na kutoa ule ambao uko kwa jicho. Hii ni kwa sababu mshale ukiwa kwa jicho unahitaji uwe makini zaidi. Unaweza kutoa ule ambao uko kwa tako lako bila kufikiria sana. Hivyo ndivyo watu wa Rwanda walifanya. Waliweza kukosoa yale mambo ambayo yalifanya kuwe na mauaji ya halaiki mwaka wa 1994. Walikomesha mauaji hayo kama wametengwa. Hata aliyekuwa kiongozi wa Umoja wa Kimataifa, Bw. Kofi Annan, alihuzunika sana kwa sababu nchi nyingi ziliwaangalia wakiuana na wakawatenga. Lakini wameweza kutatua shida zao kwa miaka 20 iliyopitia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}