GET /api/v0.1/hansard/entries/476238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 476238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/476238/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Imekuwa safari ngumu kwa Wanyarwanda, lakini wameonyesha kwamba wanaweza kusuluhisha haya mambo. Bw. Spika wa Muda, niliweza kuhudhuria ibada kanisani kule Rwanda. Niliambiwa kuwa wengi wa wahubiri makanisa huko ni Wakenya. Pia wafanyabiashara wengi kule ni Wakenya. Niliona Benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) na Equity kutoka hapa Kenya. Haya ndio mambo ambayo tunafaa kudumisha. Si lazima twende mbali sana kutafuta kazi kwa watu wetu. Walimu wengi sana kule Rwanda ni wa kutoka Kenya. Ni lazima tushukuru na kuhakikisha kwamba tunadumisha uhusiano wetu na Rwanda. Kuna mambo ambayo ningetaka pia sisi tuyasome kutoka kwa Wanyarwanda. Ukitembea Mji wa Kigali utagundua kuwa ni mji ambao ni msafi sana ukiulinganisha na miji ya Nairobi na Mombasa. Sisi tuna tabia ya kutupa takataka kila mahali. Mji wa Kigali umepiga hatua kwa kuhakikisha ya kwamba ni mji msafi. Huwezi kuwapata watu wakitupa takataka ovyoovyo kama tunavyofanya hapa. Hata duka la Nakumatt ambalo liko kule halina mifuko ya plastiki. Sisi tumejaribu kufanya hivyo hapa na tumeshindwa. Kila siku watu wanakufa kutokana na magonjwa ambayo yanaletwa na takataka. Tumetembea kule Rwanda na kuona vile mambo yanafanyika na naamini kwamba mambo haya yanaweza kufanyika pia hapa nchini. Bw. Spika wa Muda, tunaweza kusoma mambo mengi, lakini la muhimu ni kuwa ni lazima sisi, kama viongozi, tujue kwamba ni lazima Serikali ishirikiane na watu. Rwanda imefika mahali hapo kwa sababu ya watu wote kushirikiana bega kwa bega. Nilipata nafasi ya kutembea hata vijijini na vitongoji kule Kigali na hata karibu mpaka kwa Rwanda na Congo. Kuna umoja ambao sisi kama Wakenya hatujapata. Vikao vya vijiji vilitengenezwa na kuwahusisha hata wale ambao walitekeleza mauaji, manusura na waliopoteza familia zao. Watu waliweza kuongea na kusikizwa. Tunafaa kujifunza kutokana na jambo hili. Tunafaa kujua kwamba yale maneno ambayo tunasema kama viongozi yanaweza kuunganisha au kuwatenganisha Wakenya. Vitabu vikiandikwa miaka 20 au 30 ijayo, jina la mtu halifai kuwa kwa vitabu hivyo kama huyo mtu alitoa matamshi ambayo yalifanya watu wapigane. Pia tusifikirie kwamba Kenya haiwezi kuwa na mauaji ya halaiki. Ungewauliza Wanyarwanda siku kadhaa kabla ya mauaji hayo hawangefikiria kwamba mauaji hayo yangefika kiwango hicho. Ilianza kama mzaha, kisha ikawa ngumu kusitisha. Ni lazima tujifunze kama wananchi. Bw. Spika wa Muda, namshukuru Rais wa Seneti ya Rwanda kwa kutuhutubia. Naamini kwamba tutaendelea kushirikiana kwa mazuri na kusoma yale mabaya na kuyasema vile yalivyo. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}