GET /api/v0.1/hansard/entries/477577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 477577,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/477577/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Simba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 12532,
        "legal_name": "Paul Simba Arati",
        "slug": "paul-arati-simba"
    },
    "content": "Hoja ya nidhamu, mhe. Spika. Kufuatana na Kanuni No.44, ningetaka kuguzia swala ambalo limekuwa katika vichwa vya habari na katika magazeti kuhusu hali yangu ambayo imesemwa nina bunduki. Inadaiwa kwamba nilitoa bunduki na kutaka kumpiga risasi mfanyabiashara mmoja. Nataka kusema kwamba huo ni uongo mtupu. Mimi sijawahi kuwa na bunduki. Sijawahi kupewa leseni ya kubeba bunduki na sijui kutumia bunduki. Nataka niseme kwamba haya yamefanyika katika eneo la Bunge langu ambapo kumekuwa na mzozo wa ardhi ambayo Marehemu Wangari Maathai alikuwa amesimamisha ujenzi wake. Tarehe 11th May, nikiwa na Mbunge, hon. Mutemi tukiwa kule Dagoretti, niliitwa kwa sababu lile shamba lilikuwa limeingiwa na vijana kutoka eneo langu la Bunge. Walikuwa kadiri ya vijana kumi. Nilipoingia pale, wale niliwakuta pale, wawili wa vijana hao walitoa bunduki na alipotaka kunipiga risasi, yule mlinzi wangu aliingilia kati. Alitoa bunduki yake na kukawa na sitofahamu hadi yule mtu akarudisha bunduki yake mfukoni. Huyo mfanyabiashara anadai kwamba analindwa na polisi na akataja majina ya wakubwa. Alimtaja mkubwa wa CID ambaye nilienda kumwona. Mkubwa wa CID, Bw. Muhoro akakataa. Akasema mtu yeyote ambaye ni mwarifu lazima akamatwe na ashtakiwe."
}