GET /api/v0.1/hansard/entries/479362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 479362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/479362/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S. A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kupata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya utawala na usalama wa kitaifa kuhusu mikakati ambayo Serikali imeweka kuzuia janga jingine kwa kuwa imesema kwamba tatizo hili, ama yale yaliyotokea Mpeketoni, lilitokana na Al Shabaab. Tukizingatia kwamba eneo la Ubunge la Lamu Mashariki linapakana na Somalia pale Kiunga, Serikali imeweka mikakati gani kuhakikisha mpaka ule wa Kiunga umekuwa na usalama? Hii ni kwa sababu tunadhani kwamba Al-Shabaab wanatoka Somalia. Mpaka ule wa Kiunga hivi sasa uko hali gani ya kiusalama? Usalama uko Mpeketoni pekee kwa sababu ya yale yaliyotokea ama Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba katika mpaka ule kuna usalama wa kutosha, na kwamba tukio kama hilo haliwezi kutokea tena katika siku zajazo."
}