GET /api/v0.1/hansard/entries/48098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 48098,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/48098/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Ahsante, Bi. Naibu wa Spika wa Muda kwa nafasi hii muhimu ya kutenda kazi iliyonileta katika Bunge hili. Kwanza, ningependa kumshukuru mhe. Ababu na kumwambia kwamba ushujaa wa kiongozi ni kutenda matakwa ya uwakilishi wa watu waliomleta hapa. Maisha yanayopotea mikononi mwa askari; maisha yanayopotea mikononi mwa magaidi; na maisha yanayopotea kwa njaa hayana tofauti. Kila Mkenya ana haki ya kulindwa na Serikali. Kama ulinzi unaotaka wewe ni wa kuhakikishiwa maisha mema ni lazima hilo lifanyike. Hii ni kwa sababu hiyo ni haki ya kikatiba ambayo Mkenya amewekewa. Niko tayari kunukuliwa. Ukiangalia bajeti za nchi hii, vitengo vya Serikali, kwa mfano, vitengo vya kupigana na ugaidi, jeshi, na intelligence vina bajeti kubwa sana kwa kusudi la kulinda maisha ya Wakenya. Janga la ukame si jambo jipya hapa Kenya. Janga hili huja kila mwaka. Sisi wengine tunahakika kwamba mwakani ikiwa tungali Bunge hili tutayazungumzia mambo haya kuhusu janga la ukame na njaa. Serikali iliyoko kweli ina pande mbili lakini siyo Serikali ya mkoloni ama mtu ambaye si Mkenya. Waziri Mkuu ni Mkenya na Rais Kibaki ni Mkenya. Wamechaguliwa na Wakenya kulinda na kuangalia matakwa ya Wakenya."
}