GET /api/v0.1/hansard/entries/48105/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 48105,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/48105/?format=api",
"text_counter": 314,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, nakushukuru kwa muda huu ulionipatia. Ninaomba nichangie kwa kumpongeza mhe. Namwamba kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Yangu ni machache. Tumeona Serikali ikilaumiana huku na kule. Ninaiomba Kamati hii inayoundwa iangalie kwa undani na iweze kujua ni nani anayeiba mafuta, na ni kwa sababu gani hatuna mafuta ya kutosha. Kamati hii inabuniwa wakati unaofaa, ili tupate kujua chanzo cha matatizo yanayoikumba nchi hii. Kuna mambo mengi yanayotokea katika nchi hii, ambayo hatuelewi. Hatuelezwi. Kuna ufisadi. Mambo yamefichwa. Tungependa yafafanuliwe. Kamati hii itakuwa na jukumu la kuja Bungeni na kuielezea nchi,kwa jumla, juu ya ufisadi unaoendelea. Watu wanaleta mafuta halafu wanayaficha. Watu wanashindwa kusafiri. Gharama za usafiri zimekuwa za juu, na watu hawawezi kufanya shughuli zao. Jambo hili limechangia sana kupanda kwa bei za chakula. Hakuna chakula nchini. Imekuwa shida kwa mtu kusafirisha mboga zake kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa sababu ya gharama za juu za usafiri. Tunaiomba Kamati hii pia iangalie kwa undani ni vipi tunaweza kuzipunguza gharama hizi ili wananchi wapate nafasi ya kufanya shughuli zao. Bi. Naibu Spika wa Muda, pia, ninaomba nigusie suala la wazee."
}