GET /api/v0.1/hansard/entries/48116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 48116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/48116/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Yakub",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 378,
"legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
"slug": "sheikh-dor"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na mhe. Namwamba. Ningetaka Serikali ichukue jukumu la kupunguza kodi inayotozwa umeme na mafuta. Ningeomba pia iwaruhusu wanabiashara wote ambao waonaweza kuleta mafuta wafanye hivyo ili bei ya mafuta iwe nafuu kwa mwananchi wa kawaida. Ningeomba Kamati hiyo ishughulikie wafanyikazi ambao wamepewa nyongeza ya asilimia 12 ambapo gharama zimepanda kwa asilimia 25. Pia, ningeomba Serikali iwasaidie wakulima, wavuvi na wafugaji. Ningeomba pia Serikali iwasaidie vijana kwa kubuni nafasi za kazi. Bi. Naibu Spika wa Muda, ikiwa Serikali itajishughulisha na maswala haya, gharama ya maisha itapungua maradufu. Swala la afya ni muhimu sana kwa wananchi wetu. Ninaomba Serikali iimarishe afya ya wananchi wake. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}