GET /api/v0.1/hansard/entries/481373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 481373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/481373/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa usia ambao umeutoa leo. Ilani imeshatolewa kwa muundo msingi ambao umewekwa wakfu hasa kwa kutekeleza na kuunda kamati ya halmashauri ya maeneo ya ugatuzi katika kaunti. Tunajua kwamba wiki hii, magavana walikutana na kuafikiana kwamba hawataheshimu wala kuhudhuria vikao vya kamati hii. Ningetaka wajue kwamba kuna sheria. Korti haijaamua kwamba sheria haitafanya kazi. Ni jukumu lao kuheshimu sheria. Jana, niliongea na Gavana wa Migori na hatukuafikiana. Alianza kuteta nami nikamwambia sheria ni lazima itekelezwe. Wakati wa mtu mmoja kuamua maendeleo na utekelezaji umepita. Tungetaka kuona Migori ikionekana Kenya nzima kwamba ina mipango kamili inayotekelezwa kwa utaratibu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}