GET /api/v0.1/hansard/entries/481454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 481454,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/481454/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Spika, wahenga walisema: “Hayawi hayawi huwa.” Methali hii si hadithi za Alfu Lela Ulela, Hekaya za Abunuasi au ngano za paukwa pakawa. Hoja hii imetokana na utundu na utenda kazi duni wa magavana wetu ambao hawafuati sheria kama ilivyoandikwa katika Katibu yetu. Ni aibu kubwa kwamba leo, katika Seneti hii, tunazungumza juu ya Gavana Isaac Ruto, Jack Ranguma, William Kabogo na Mwangi wa Iria kwa kutokuwa na nidhamu ya kuheshimu sheria na mujibu uliowekwa katika Katiba yetu. Tabia yao mbaya yakutothamini sheria imeweka hatarini maeneo yao ya utawala na hawatapewa hela kipande cha pili. Juzi, walienda kortini na kupewa asilimia 50 za kugawa pesa mwaka huu. Wanaweza kuringa kwamba wana hela. Lakini, kuna mgao wa pili; asilimia 50 ambao umesimamiwa na Seneti hii. Hawatakuwa na nguvu za kuchukuwa pesa hizo kwa minajili ya maendeleo hata kulipa mishahara katika sehemu zao za kazi. Hii ni aibu kubwa ambayo wanaleta kwa uandaliaji wa mipango mizuri ya maendeleo ya maeneo ya kaunti. Labda baada ya kuongea tutapitisha kauli ili wasipewe ruhusa ya kuzichukua hela hizo kwa minajili ya kazi yoyote. Lakini naomba wakimbie hima iwezekanavyo ili wafike kwa kamati hii ya kusikiliza mashtaka ambayo tumeyapata. Si sisi tuliyowasilisha mashtaka hayo. Haya ni mashtaka ambayo yametoka kwa yule katibu karani mkuu wa hela za serikali. Kuna mambo hapa. Hela za Serikali hazikutumika vizuri. Hela za uma hazikutumika vizuri katika maeneo ya magavana hawa. Wanafaa kuleta stakabadhi ambazo walizonazo na kueleza kikao hiki ambacho kiliwaomba kufika kwa heshima taadhima, mara mbili, tatu hadi tisa. Wengine wamepata nguvu za kuandikia kamati hii ambayo imeundwa na sheria ya Kenya. Hili ni jambo la ufidhuli na unafiki kwamba hawa wameanza kujifanya wafalme. Wamesahau kuwa wao ni watumishi wa wananchi. Bw. Spika, natoa mwito kwa magavana wa sehemu nyingine iliwajue kwamba sheria ipo. Vipengele vipo na vyote vilisomwa hapa na mhe. (Dr.) Khalwale. Alivisoma vipengele 99, 93,229,125 vya Katiba na hasa kile cha nguvu zaidi, kile cha 225 ambacho kinaipa Seneti hii nguvu za kusimamisha utoaji wa hela kwa sehemu hizi. Litakuwa ni jambo la kusaga meno na kulia ikiwa wale wachache na wengi waliowachwa mashinani hawatajua kwa nini mipango yao ya kimaendeleo imekatizwa. Ni kwa nini mishahara yao imesimamishwa na kadhalika? Hii ni kwa sababu ya uzembe, ujeuri na kutokutii kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}