GET /api/v0.1/hansard/entries/481457/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 481457,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/481457/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika ninakushukuru kwa nafasi hii ili niweze kuunga mkono Hoja hii ambayo ni ya maana sana. Vile vile nimefurahishwa kwa sababu matamshi yako ya hapo awali yameweza kutuelekeza pahali tunataka kuelekea. Kwa ufupi, ningetaka kusema ya kwamba, sisi wote tulioko hapa tulichaguliwa na kura ya mwananchi. Kura tuliopigiwa ilikuwa ni ili tuitumikie Taifa letu. Jambo la kushangaza ni sarakasi na kassheshe ambayo inaendeshwa na magavana. Hivi leo, Seneta hawezi kusimama katika kaunti yake na kusema, kwa mfano, pesa yetu ilikuja kiasi fulani na imetumika kiasi fulani. Hawa magavana wamejitunukia madaraka ambayo hawajapewa na mwanchi wala Katiba. Sen. (Dkt.) Machage amesema kwamba wameajiri mabibi wao na mtu mwingine hawezi kupata kazi. Gavana anataka aitwe Mtukufu na mke wake ni Mtukufu Mke wa kwanza wa Kaunti. Kuna moja wa CEC alifutwa kazi kwa sababu alisimama na kuwatambua kama Mhe. Gavana na mke wake. Alikosa kusema Mhe. Mtukufu Gavana na Mhe. Mtukufu Mama wa Kwanza wa Kaunti. Hivi leo, Wawakilishi wa Wadi (MCAs) hawakai katika vikao vya mpangilio wa bajeti ambayo inapangwa katika kaunti. Inapangwa na Gavana na chokora wake ambao amechagua na kuwaweka kuwa CECs. Hiyo bajeti ikitoka pale, hakuna Mbunge anayehusika. MCA hajui ni jambo gani linatendeka. Bw. Spika, uongozi umetoka kwa Serikali kuu hadi kwa Gavana. Kwa hivyo, ili tuweze kupiga hatua na kuenda mbele, inafaa tuunge mkono Hoja hii kwa sababu inafutana kwa karibu na zile kamati ambazo tutatengeneza za maendeleo. Katiba imesema kwamba kazi ya Seneti hii ni kuangalia, kufuatilia na kusimamia vile hela za umma zinatumika, halafu Kamati ambayo imetengenezwa kulingana na sheria ya Taifa hili inaandika barua kwa Gavana kumuuliza kufika kwa Bunge kwa sababu mgaguzi wa hesabu ya kitaifa ameweza kuonyesha kwamba kuna uporaji ama uharibifu wa fedha, na Gavana anadinda kufika. Badala yake anamtuma karani ama katibu wake kuhudhuria kikao hicho. Rais wa nchi hii mwenyewe nililimnukuu akisema kwamba akiitwa na kamati yoyote atahudhuria. Kama Rais wa nchi anasema wazi wazi na katka uwanja wa kitaifa akihutubia wananchi ya kwamba akiitwa atahudhuria, unawaweza kufikiria magavana wana hadhi ya juu kuliko Rais wa Taifa. Mmoja ameunda akaunti yake ya benki ya kutumia pesa za kibinafsi ambayo ni ya kisiri, na alipoulizwa ni kwa nini ana hiyo akaunti, alisema kwamba, hakuna mtu ambaye anauliza Rais Kenyatta kuhusu akaunti yake ya kibinafsi. Ninaunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}