GET /api/v0.1/hansard/entries/482376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 482376,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/482376/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe mchango wangu kwa Mswada huu wa Mapato. Huu ni Mswada muhimu sana kwa nchi yetu na unafaa uangaliwe kwa makini sana. Kila Mbunge anahitajika na anatakiwa atafakari ni wapi Mswada huu unatupeleka na matokeo yake yatakuwa yapi. Nikitoa maoni yangu kuhusu Mswada huu, naomba nichukue nafasi hii kwanza, kukishukuru chama changu cha Orange Democratic Movement (ODM) na muungano wa CORD kwa ujumla kwa kunitunukia nafasi ya kuwa kiranja wa walio wachache Bungeni na walio wengi nchini. Hii ni kwa sababu sisi ndio tulio wengi nchini lakini hapa Bungeni, tuko wachache. Natumaini kwamba ndugu zangu wa muungano wa Jubilee wanaelewa huo msimamo."
}