GET /api/v0.1/hansard/entries/482379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 482379,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/482379/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Na tuliongeza mmoja jana, ijapokwa sikuwa hapa nchini. Tumeongeza moja kutoka eneo la Uwakilishi Bungeni la Mathare. Nashukuru kila mmoja aliyehusika na shughuli hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimshukuru aliyekuwa kiranja wa walio wachache Bungeni, Mhe. Mung’aro kwa kazi alizozifanya wakati alikuwa katika kiti cha kiranja wa walio wachache Bungeni. Namshukuru kwa kazi zake na namtakia kila la heri. Naomba wenzangu wa muungano wa CORD tushirikiane na tuangalie hawa ndugu zetu wa Muungano wa Jubilee. Tunaenda nao kwa safu moja kwa moja. Pale ambapo hawatekelezi wajibu wao, tunawakosoa yakutosha kwa sababu ni wajibu wao. Mara nyingi, kuna utelezi na utetezi. Ni wajibu wetu sisi ambao tuku katika upande huu, pale ambapo mambo hayakuenda sawa sawa, turekebishe. Siyo kwa ubaya wala utata ama ugomvi. Mhe. Naibu Spika, naomba tushirikiane na wenzetu kujenga nchi yetu. Tulipitisha Mswada wa ugawaji wa fedha unaoitwa Appropriation Bill; kodi zitakazotumiwa. Ilikuwa tuangalie zitatumiwa namna gani. Ni njia gani tutatafuta mapato na ni mbinu gani tutakazotumia ili nchi iweze kupata mapato ya kutosha. Ni muhimu pia njia hizo ziambatane na uchumi wa nchi. Ni muhimu pia ziangalie kuwa watu wako katika nafasi gani ya kuweza kutoa fedha hizo. Mhe. Naibu Spika, utakubaliana nami kwamba si kila wakati ushuru ukichukuliwa ama tukichukuwa nafasi zile zinatumiwa kwa kutafuta ushuru, nchi itakuwa nzuri. Tukiangalia hali ilivyo katika nchi ambazo zimeendelea, utakuta nchi kama Ujerumani, Sweden, Denmark, Uingereza na hata Marekani, ushuru wao ni wa hali ya juu, mradi tu unatumiwa vyema. Tungeomba kwamba Mswada huu ambao umekuja uangaliwe kwa makini. Hela ama fedha zikitafutwa zinatumiwa kwa njia gani? Mara nyingi, utakuta fedha zinatafutwa na watu wanatoa ushuru. Lakini jinsi zinavyotumiwa, hazilingani wala hazisaidii nchi. Mara nyingi utakuta kwamba kuna uporaji mwingi sana wa fedha za umma. Utekelezaji wenyewe wa miradi ambayo inafadhiliwa na fedha hizo upo na kasoro nyingi. Watu wakiulizwa waeleze ama waajibike sawa sawa ama wazi wazi, mara nyingi, wanaona kama wanaonewa. Lakini ukweli ni kwamba watu wengependa watoe ushuru na mapato yaongezeke. Lakini vile fedha zinavyotumiwa hailingani na mahitaji ya watu. Watu wachache ndio wanajinufaisha na fedha hizo. Ni sehemu chache tu za nchi zinapata maendeleo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}