GET /api/v0.1/hansard/entries/482380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 482380,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/482380/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, tukiangalia Mswada huu katika kipengele cha pili hadi cha 24, vipengele hivi vyote vimependekeza mageuzo fulani ya kutafuta ushuru. Mbinu hizi ni muhimu. Hizi mbinu zilingane na mahitaji ya nchi. Hizi mbinu za kutatufa hela ni muhimu. Lazima tuzingatie vile tutakavyoweza kuinua kiwango cha maisha cha watu wetu. Tukiangalia nchi nzima, utakuta kwamba, mara nyingi, usambazaji wa miradi umegemea upande fulani. Tungependa kurekebisha hayo na ndio maana tukaomba ugatuzi katika Kenya. Ijapokuwa ugatuzi umeingia, bado kuna changamoto za vile hela zinavyotumiwa mashinani, hasa tukiangalia vile magavana wengine wanavyotumia pesa. Hawataki kujibu vile fedha zinavyotumiwa.. Mhe. Naibu Spika, singependa kutumia muda mwingi, ijapokuwa tu kuzungumzia kwa uchache kuhusu NSSF. Inapendekezwa isimamiwe na RBA kulingani na vile Katibu Mkuu wa COTU alivyotoa maoni yake. Lakini si Serikali ichukue uenezaji na mamlaka ya kuhakikisha kwamba wale watu ambao wanawakilisha wafanyikazi hawapewi nafasi. Mhe. Naibu Spika, tusipokuwa waangalifu, tutalenga kupandisha ushuru kwa vitu ambavyo vinahitajika na wananchi kila wakati wa maisha yao. Mara nyingi, wananchi wanaathirika na hawapati afueni ya kuweza kuhimili maisha. Kwa hivyo, ni ombi langu kwamba tunapotoa mapendekezo haya, yaweza kubainika wazi kuwa yatakuwa yanafaa nchi na yataweza kusaidia nchi kwa ujumla. Kwa hayo mengi, nilikuwa nje ya nchi na nashukuru Mungu nimerudi salama. Nitatekeleza wajibu wangu kulingana na kanuni za nchi na za Bunge na kila mtu aelewe kwamba, ukiwa kiranja Bungeni, kuna matarajio wenzangu wanatarajia kutoka kwangu. Ningependa kuwahakikishia wenzangu kwamba nitatimiza wajibu wangu kwa mjibu wa sheria. Na yale wanaotarajia kutoka kwangu kama kiranja, nitayatimiza. Wasiwe na wasi wasi. Na wenzangu katika upande wa Jubilee, mwe sawa sawa kwa sababu tutaonana ana kwa ana! Ahsante."
}