GET /api/v0.1/hansard/entries/484387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 484387,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/484387/?format=api",
"text_counter": 488,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika nimekaa hapa kwa utulivu nikisikiza mawaidha ya Maseneta wezangu kuhusu mashtaka ya Bw. Naibu Gavana. Kuna mnyama anayeitwa fisi. Mnyama huyu anapenda sana kula nyama. Aonapo nyama ya tumbo lake mwenyewe, anaanza kuikula mpaka anakufa kwa sababu ya tamaa yake. Seneti hii haifai kuwa hivyo. Tusifikiri kwamba kwa sababu kuna shida, kuna nafasi ya kula na kuchafua jina la Bunge. Mkuki kwa nguruwe ni mtamu lakini kwa binadamu ni mchungu. Huyu nguruwe, kwa mfano, labda ni Naibu wa Gavana ambaye yuko hapa leo. Bw. Spika, kwa hivyo uamuzi wako ni lazima uwe wa hekima siku ya leo. Hii ni kwa sababu itaandikwa kwa historia ya Seneti na kusomwa, kwamba Spika wa Seneti, ambaye kwa miaka karibu miwili ametoa uamuzi wa haki, hivi leo ameamua vingine. Haijulikani kura zetu zitaenda wapi. Wao wanahesabu tu na kuamua kuwa wale walioko upande wa kushoto ni wapinzani. Je, unajua ningepiga kura vipi? Wangevumilia chuma kiive. Lakini sasa kwa sababu wamedhihirisha na kuthibitisha uoga hadharani, mbele ya vyombo vya habari na Kenya nzima--- Wakenya wamesoma na wanaona kile kinachoendelea katika Seneti hii hivi sasa. Bw. Spika, kwa hivyo nakusihi kwa hekima yako, ukiwa kiongozi wetu tunayempenda, kwamba ingawa umetoa hukumu hapo awali kwamba tungoje siku The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}